Wakazi wa jiji la Mbeya wamejitokeza kwa wingi katika stendi kuu mpya iliopo eneo la nane nane RRM kwaajili ya kuomba maeneo ya kufanyia biashara zao katika eneo hilo.Wageni kutoka mikoani mnataarifiwa kua stendi kuu ya jiji la Mbeya kwa sasa ipo eneo la nanenane (karibu na Uyole) na si mjini soko matola tena kama iliyokuwa hapo awali,lakini si wa mikoani tu bali hata baadhi ya wilaya za jiji la Mbeya.Hivyo ukifik jijini Mbeya usishangae kuambia kuwa basi linaishia hapo eneo la Nane nane,kwani ndipo ilipo Stendi Kuu mpya kwa sasa na siku zote.
Muonekano wa eneo la Stendi kuu hiyo.
Abiria wakisubiria Usafiri kwenye stendi kuu hiyo.
Sehemu ya kuingilia Mabasi.
Mabasi madogo yanayofanya safari zake katika baadhi ya Wilaya za Jiji hilo la Mbeya.
Sehemu ya Wakazi wa Jiji la Mbeya waliojitokeza kwa ajili ya kuomba maeneo ya kufanyia biashara zao kwenye Stendi kuu Mpya ya jiji la Mbeya.Picha zote na Fadhil Atick - Globu ya Jamii,Mbeya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 02, 2014

    Hii stendi ya Mbeya ni ya kisasa inatia moyo wale ambao stendi zao vumbi tupu wanatakiwa kujifunza hapo. Watendaji wote wangekuwa na maono ya maendeleo Tanzania tungekuwa mbali. Tunatarajia maendeleo zaidi onyesha njia Mbeya tunahitaji pia shopping mall ya uhakika Mbeya mjini. Tunawapongeza watendaji kwa kazi hii, ila maelekezo ya kiswahili yawepo pia.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 03, 2014

    Bado inahitaji maboresho makubwa.kama sehemu ya kuwakinga abiria na mvua au jua nk...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...