Nimesoma habari gazeti la UHURU la leo tarehe 9 Julai,2014 lenye kichwa cha habari TRA YAZUIA GARI LA NAIBU WAZIRI.Adaiwa kukwepa kulipa kodi kwa miaka miwili kodi ya leseni ya barabara.
Nachukua fursa hii kukanusha habari hizo kuwa ni za uongo zenye hila na mwelekeo wa kisiasa kwa aliyeandika kwa makusudi kwa lengo la kunichafua na kunishushia heshima yangu.Habari iliyoandikwa imejaa uzushi,hila na upungufu mkubwa wa kimaadili ya kiuandishi wa habari.
NAOMBA uuma wa watanzania kujua yafuatayo:

1.MIMI AMOS GABRIEL MAKALLA si mmiliki wa gari tajwa noT534BFP
2.Kodi inayodaiwa sh 662,500(laki sita sitini na mbili elfu mia tano tu) kwa mujibu wa taarifa za mwenye gari mpaka habari hii inaandikwa zilikwisha kulipwa.
HIVYO BASI,kutokana na ukweli huo habari hii ililenga kunichafua kwa makusudi na ina chembechembe za kisiasa na hila dhidi yangu na  kwa uzito huo
1.Nimemwagiza mwanasheria wangu AMICUS Advocates kuwaandikia gazeti la UHURU,MHARIRI na MWANDISHI WA HABARI HII kuniomba radhi  NDANI YA siku SABA kwenye ukurasa wa mbele wa gazeti  kwa matoleo MATATU MFULULIZO 
2.Kinyume na hilo nawashitaki gazeti,mchapishaji,mhariri na mwandishi na kunipa fidia Tshs 1,000,000,000(Tshs Bilioni moja tu)
NARUDIA kusisitiza kuwa uandishi wa aina hii si tu unatia mashaka taaluma ya mwandishi aliyeandika bali pia ametumia kalamu yake kufanya siasa za maji taka na ili ukweli ujulikane nawakaribisha mahakamani ...
asanteni
AMOS G MAKALLA
Mbunge mvomero na naibu waziri maji

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...