KATIKA TUKIO LA
KWANZA:
MTU MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA RAHABU KIHANIKU (60)
MKAZI WA KIJIJI CHA KIKOTA AMEFARIKI DUNIA MUDA MFUPI BAADA YA KUFIKISHWA HOSPITALI YA SERIKALI MAKANDANA – TUKUYU KWA MATIBABU
BAADA YA KUGONGWA NA PIKIPIKI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.343 CMQ AINA YA HONDA
ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA NDULA
MWASANGAJA (32) MKAZI WA MTAA WA
BAGAMOYO –TUKUYU.
AJALI HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 30.06.2014 MAJIRA YA SAA
06:00 ASUBUHI KATIKA KIJIJI CHA KIKOTA, KATA YA KIWIRA, TARAFA YA UKUKWE,
WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA KUU YA MBEYA/TUKUYU.
AIDHA KATIKA AJALI HIYO MTOTO
ANGEL OSWARD (02) MKAZI WA
KIKOTA ALIYEKUWA AMEBEBWA NA MAREHEMU AMEVUNJIKA MGUU WA KUSHOTO NA AMELAZWA
HOSPITALI YA SERIKALI MAKANDANA –
TUKUYU. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. MTUHUMIWA AMEKAMATWA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA
POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO
KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA
ALAMA ZA USALAMA ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA
WATEMBEA KWA MIGUU KUTEMBEA PEMBEZONI MWA BARABARA NA KUVUKA MAENEO YENYE VIVUKO
[ZEBRA CROSSING] ILI KUEPUKA AJALI.
KATIKA TUKIO LA
PILI:
MTU MMOJA AMBAYE HAJAFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE, JINSI YA KIUME,
MWENYE UMRI KATI YA MIAKA 19-20
AMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA
DEREVA ASIYEFAHAMIKA.
AJALI HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 30.06.2014 MAJIRA YA SAA
22:14 USIKU KATIKA MTAA WA MBILINYI - SAE, KATA YA ILOMBA, TARAFA YA
IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. MTUHUMIWA
ALIKIMBIA NA GARI MARA BAADA YA AJALI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI
YA RUFAA MBEYA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA
POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO
KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA
ALAMA ZA USALAMA ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE
MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA
HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE, VINGINEVYO
AJISALIMISHE MWENYEWE.
TAARIFA ZA MISAKO:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU SABA KWA KOSA LA
KUPATIKANA NA BHANGI. WATUHUMIWA HAO NI PAMOJA NA 1. JELY EVARIST (24) MKAZI WA MWANJELWA 2. STAFORD NGENZI (21) MKAZI WA MWANJELWA, 3. ALAN AGUSTINO (23) MKAZI WA ILEMI 4. ASIFIWE ABSOLOM (22) MKAZI WA JUA KALI 5. DATI SAMWEL (24) MKAZI WA MWANJELWA 6. MWAKISYE NAZARETH (23) MKAZI WA MWANJELWA NA 7. MICHAEL EZEKIEL (40) MKAZI WA NZOVWE.
WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA KATIKA MAENEO TOFAUTI JIJINI MBEYA WAKIWA
NA BHANGI YENYE UZITO WA GRAM 429. MSAKO
ULIFANYIKA KATIKA MAENEO YA JUA KALI, MAKUNGULU NA MAJENGO MAPYA, KATA ZA ILEMI
NA NZOVWE, TARAFA ZA SISIMBA NA IYUNGA MNAMO TAREHE 30.06.2014 MAJIRA YA SAA 23:30. WATUHUMIWA NI WATUMIAJI NA WAUZAJI
WA BHANGI.TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA
POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO
KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI
HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII KUTOA
TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ZA WATU AU MTANDAO WA WATU WANAOJIHUSISHA NA
UUZAJI NA USAMBAZAJI WA DAWA ZA KULEVYA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA
ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
Imetolewa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...