Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mkuu mstaafu wa Zanzibar Hamid Mahmoud Hamid akizungumza mjini Babati na waandishi wa habari wa Mkoa wa Manyara(hawapo pichani) , juu ya maandalizi ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia teknolojia ya Biometric Voter Registration (BVR) unatarajia kuanza mwezi Septemba mwaka huu (kushoto) ni Mkurugenzi wa sera na mipango wa Tume hiyo Eugenia Mpanduji na kulia ni Mkurugenzi wa Mji wa Babati Bw. Omary Mkombole.
Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Eugenia Mpanduji akizungumza mjini Babati na waandishi wa habari wa Mkoa wa Manyara, juu ya maandalizi ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia teknolojia ya Biometric Voter Registration (BVR) unatarajia kuanza mwezi Septemba mwaka huu (kulia) ni Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Mkuu mstaafu wa Zanzibar Hamid Mahmoud Hamid.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...