Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF umeajiri
Wataalamu waelekezi ( TA) ambao watatoa huduma katika halmashauri mbalimbali
nchini kwa lengo la kusimamia ipasavyo shughuli za Mpango wa kunusuru kaya
masikini na zinazoishi kwenye mazingira hatarishi PSSN.Watalaam waelekezi hao
wako katika mafunzo kwenye ukumbi wa CEEMI jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo
ya Jamii TASAF ,Ladislaus Mwamanga (wa nne kutoka kushoto) akiwa katika picha
ya pamoja na baadhi ya Wataalam Waelekezi wapya (TA)ambao wako katika mafunzo
ya namna ya utekeleza majukumu yao katika Mpango wa Kunusuru Kaya masikini PSSN
ulioko chini ya TASAF awamu ya TATU. Walioketi ni baadhi ya wakurugenzi na
mameneja wa TASAF.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF ,Ladislaus Mwamanga
(aliyesimama) akitoa hutuba ya ufunguzi wa mafunzi ya Wataalam Waelekezi (TA)
walioajiriwa na TASAF kwa ajili ya kuhudumia Halmashauri za wilaya mbalimbali
nchini (hawapo pichani)ikiwa ni mkakati wa kufanmikisha Mpango wa kunusuru kaya
masikini nchini.
Baadhi ya wataalamu Waelekezi TA wapya
walioajiriwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF wakisikiliza hoyuba ya
ufunguzi wa mafunzo yao katika ukumbi wa CEEMI ambayo ilitolewa na Mkurugenzi
Mtendaji wa TASAF ,Ladislaus Mwamanga hayupo pichani ambaye pamoja na mambo mengine alisistiza
umuhimu wa wataalamu hao kufanya kmazi kwa uaminifu na kujituma na kushirikisha
sekta nyingine kwenye halmashauri watakazopangiwa.
Baadhi ya Wataalam waelekezi wapya (TA ) watakaotoa huduma katika
halmashauri mbalimbali nchini wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bwana
Ladislaus Mwamanga hayupo pichani wakati alipofungua mafunzo elekezi ya namna
ya kutekeleza majukumu yao kikamilifu kwa lengo la kufranikisha Mpango wa
Kunusuru Kaya masikini nchini,PSSN.
Meneja Rasilimali watu wa Mfuko wa
Maendeleo ya Jamii TASAF Bi Thecla Makundi
(aliyeshika tama)akimsikiliza kwa makini mmoja wa Wataalamu Waelekezi wapya
alipokuwa akitoa maelezo katika mafunzo ya watalaam hao yanayofanyika kwenye
ukumbi wa CEEMI jijini DSM.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...