MHE IDDY SANDALY

Katika Historia ya DMV kwa Miaka miwili mfululizo ya Uongozi wangu  tumeweza kuwajumuisha watanzania kwenye mambo mbali mbali. Tumeweza kufanya SUMMER PICNIC kwa watanzania wote wa DMV . Tuliweza kujipanga na Kuhakikisha watoto, vijana na Wazee wanajumuishwa pamoja na kufurahia, Watanzania bila Kujali Vyama na mengineyo tuliweza kujumuika kwa pamoja na kufurahi.  Lengo DMV MOJA.

Kwa Kuendeleza kuonyesha ni jinsi Gani umoja Ndio Lengo la Jumuiya na Sio Kupata Mamilioni ya Fedha wala Kuleta Siasa au Mengineyo.Kwa Miaka yote miwili ya uongozi na Timu yangu tuliweza kuandaa Party Ya Mwaka Mpya Kwa Watanzania Wote Hapa DMV na Kwa Gharama Nafuu. Lengo ni Kushereheka kwa Pamoja na Kuwa Pamoja kama watanzania DMV. Tuliserebuka na Kulisaka Bomboka kwa Raha Zetu. Mpango Pale Pale Mwaka huu December 31, 2014.
DUAL CITIZENSHIP /HAKI YA KUZALIWA


Nimekuwa mstari wa mbele katika kulipigania swala la Dual Citizenship . Nilianzisha PETITION kwa watanzania wote ulimwenguni ili kuweza kupeleka mawazo na nguvu zetu Diaspora tulio nje Bungeni Tanzania. Petition hii nilianzisha na kuhakikisha inawafikia wabunge na Mawaziri nyumbani Tanzania ilikuweza kulisukuma swala hili la Haki ya Kuzaliwa/Dual Citizenship. Mpaka Hii leo petion hii ishatiwa sign na Watanzania 1,754, ulimwenguni. http://www.change.org/petitions/honourable-bernard-membe-we-tanzanians-in-the-diaspora-believe-that-dual-citizenship-is-a-great-thing-for-the-country-please-support

Nimeshirikiana na Viongozi wenzangu wa Jumuiya za watanzania hapa Marekani, ITALIA, IRELAND, UK, ZADIA na DIACOTA kwenye kuhakikisha swala Hili la Dual Citizenship linafanikiwa. Tumekuwa tukifanya mikutano ya Kila Jumapili kujadili na kupanga mikakati katika swala hili.  

Kwa Hivi Sasa Viongozi Wenzangu wa Jumuiya za Marekani Kwa Kazi nzuri ninayoifanya na kwa imani na uaminifu walionao juu yangu, wamenichaguwa Kuwa Mwenyekiti Wa Umoja  wa Viongozi wa Watanzania Marekani.
PESA zimekuwa zikikusanywa kutokana na MAOMBI ya muwakilishi wa wanadiaspora kwenye bunge la katiba Mr. Kadari Singo. Pesa hizi zina lengo moja tu la kuhakikisha swala hili linafanikiwa. Lengo kuu ni kuwapa semina wabunge kuhusu swala hili kama tulivyoshauriwa na Waziri wa mambo ya Nchi za Nje Bwana Bernad Membe, Mabalozi wetu na Baadhi ya Viongozi. Pia Baadhi ya Pesa zitatumika kwenye Publicity kwenye Radio, TV na nk.

Jumla ya $9,405 zimekusanywa mpaka sasa na lengo ni kukusanya $25,000 . Mimi Nilikuwa Mchangaji namba mbili (2) . Kama kuna swali wasiliana na muwakilishi wa wanadiaspora kwenye bunge la katiba Mr. Kadari Singo au kiongozi yeyote wa Jumuiya za Watanzania Marekani kwenye link hii  http://www.gofundme.com/7jtyuw.  Mr. Kadari Singo singojr@gmail.com

Matumizi yanayofanyika kwenye Pesa hizi ni LAZIMA yapitishwe na Viongozi wote wa Jumuiya hizi za watanzania. Unaweza kuwasiliana na kiongozi yeyote hapa http://www.gofundme.com/7jtyuw kwa maelezo , maoni au maswali. Pesa hizi ambazo bado ziko under gofund,com zitakuwa Transfered kwenye Jumuiya ya Hapa DMV, halafu maelekezo ya Matumizi yatafanywa na Viongozi wote. Matumizi ya $700 yalipitishwa na Viongozi wa Jumuiya za Watanzania Marekani yalifanyika, AMBAPO MIMI NIMETUMIA PESA ZANGU BINAFSI ($700) na kutumwa kwa Kaka Kadari Singo kwa Maandalizi ya awali ya swala hili la Dual Citizenship. Pesa zangu nitarudishiwa Mara tu hela zitakapokuwa Transfered kwenye account ya Jumuiya.
Kwa contacts za Viongozi wa Jumuiya za Watanzania Marekani nenda  http://www.gofundme.com/7jtyuw
Kwa mapicha kibao BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...