KAMPUNI
ya Simu Tanzania (TTCL) imetoa msaa wa vyakula kwa vituo vitatu vya
kulelea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu vya jijini
Dar es Salaam ikiwa ni kuvisaidia viweze kusherehekea vizuri siku kuu ya
Eid El Fitr.
Msaada
huo wenye jumla ya thamani ya shilingi milioni 3 umekabidhiwa na Meneja
wa TTCL, Dar es Salaam Kati, Jane Mwakalebela kwa niaba ya Ofisa
Mtendaji Mkuu wa TTCL, ambaye alisema utaratibu huo ni wakawaida kwa
kampuni yao kusaidia makundi na taasisi na idara anuai kwa masuala ya
kijamii.
Bi.
Mwakalebela alivitaja vituo ambavyo vimekabidhiwa msaada huo ni pamoja
na Kituo cha Watoto Yatima cha Mama Theresa kilichopo Mburahati, Kituo
cha Mwandaliwa cha Mbweni na Kituo cha Chakuwama cha Sinza vyote vya
jijini Dar es Salaam.
“…Msaada
huu ni maalum kwa ajili ya kusherehekea siku kuu ya Eid El Fitr, jambo
hili la leo ni utaratibu wa kampuni ya TTCL kusaidia makundi, taasisi na
idara mbalimbali kuhusu mambo yanayohusu maendeleo na ustawi wa jamii,”
alisema Bi. Mwakalebela kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk.
Kamugisha Kazaura.
Msaada uliotolewa kwa vituo hivyo ni pamoja na mchele, mafuta ya
kupikia, sukari, unga, unga wa sembe, maharage pamoja na katoni za juisi
za maboksi.
Kwa
upande wao wawakilishi wa vituo hivyo waliishukuru Kampuni ya TTCL kwa
uamuzi wake wa kuwakumbuka watoto yatima ili nao waweze kusherehekea
vizuri siku kuu ya Eid El Fitr kama ilivyo kwa familia nyingine
majumbani.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...