Mhe. OMAR Yussuf Mzee, Waziri wa Fedha, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar akiongoea siku ya jumatatu kwa niaba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati wa mkutano wa Kilele wa Baraza la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya Uchumi na Maendeleo ya Jamii ( ECOSOC). Mawaziri kutoka mataifa mbalimbali wapo hapa Umoja wa Mataifa kuhudhuria mkutano huo ambao unajadili utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya millenia ( MDGs), changamoto zake, changamoto zinazoibuka, pamoja na mchakato wa maendeleo endelevu baada ya 2015.
Ujumbe uliofuatana na Mhe. Waziri ukifuatilia hotuba yake, kutoka kulia ni Muwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi, Bi. Amina Shaaban, Katibu Mtendaji Tume ya Mipango Zanzibar, Naibu Muwakilishi wa Kudumu, Balozi Ramadhan Mwinyi na Bi. Bihindi Khatibu kutoka Zanzibar.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...