Na Mwandishi Wetu
BENKI ya CRDB imewataka wazazi kuwafungulia watoto akaunti ya Junior Jumbo kwa ajili ya akiba yao ya baadae.
Akizungumza katika maonesho ya 38 ya biashara ya Kimataifa Dar es salaam, Ofisa Masoko wa CRDB, Nazareth Kipingo, alisema akaunti hiyo ni kwa ajili ya watoto ambapo mzazi huifadhi fedha kwa ajili ya ada au akiba ya mtoto katika maisha yake ya baadae.
Alisema akaunti hiyo itamsaidia mzazi kuweka fedha kimkakati ambapo atatakiwa kutoa mara nne kwa mwaka katika msimu wa ada ya shule na kuongeza kuwa CRDB pia inaweza kumlipia mtoto ada kwa utaratibu maalum.
Kipingo alisema Jumbo junior ni akaunti inayomhakikishia mtoto elimu ya uhakika na kupunguza kero za kulipa ada kwa mkupuo kutoka mfukoni mwa mzazi.
Alisema kuwa katika maonesho hayo wanaendesha huduma za kibenki katika viwanja hivyo ili kumpunguzia mteja adha ya kutembea na pesa.

Ofisa Masoko wa Benki ya CRDB, Julius Ritte akiwahudumia wateja wapya waliofika katika Banda la CRDB kupata huduma za kibenki.
Mteja wa Benki ya CRDB akijaza fomu kwa ajili ya kufungua akaunti.
Watu mbalimbali walifurika katika Banda la Benki ya CRDB kwa ajili ya kufungua akaunti mpya pamoja na kupata huduma mbalimbali za kibenki zinazotolewa na Benki ya CRDB.
Wateja wa Benki ya CRDB wakipata huduma za kibenki kutoka katika tawi
linalotembea (Mobile Branch), wakati wa Maonesho ya 38 ya Biashara ya
Kimataifa katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...