Iddi Sandaly Mgombea nafasi ya Urais DMV

Ndugu zetu wana DMV. Kama mnavyomjuwa na kuijuwa timu Iddi (TEAM TANZANIA) kwamba huwa hatupendelei kuingia kwenye malumbano wala kwenye shutuma kwa wagombea wengine. Lakini tumeona kuna haja ya kuweka wazi au kuondoa upotoshaji wa Liberatus Mwangombe anao wafanya ninyi wana DMV, Watanzania na Wanadiaspora.

Hatutozungumzia kuhusu kikao kizima na Muheshimiwa Balozi kwani kiongozi Bora ni yule anaeweka Mijadala inayofanyika ya kuendeleza jumuiya mbele kuliko kuweka matashi na maslahi binafsi. Timu yetu inamuheshimu Balozi na Tunampongeza kwa kazi nzuri na maamuzi mazuri aliyoyafanya ili kuweza kuijenga jumuiya yetu. 

Kiufupi Maamuzi yote yaliyofikia kwenye kikao hicho yalikubaliwa na Wagombea Wote, Tume ya Uchaguzi, Bodi ya wakurugenzi ya Jumuiya na Muheshimiwa Balozi. Mkutano uliwashirikisha watu kama 20. Tunamshukuru Balozi na Maafisa wa Ubalozi kwa Kutumia Muda wao ilikusimamisha Jumuiya Yetu.

Timu Iddi Sandaly, inapend kufafanua maswala haya Matatu:

KUAHAIRISHWA KWA UCHAGUZI.

Uchaguzi uligharishwa kutoka June 20 kwenda July 21, kwa sababu wagombea wengi hawakuqualify kugombea kwa vile hawakuwa wanachama. Ndugu Liberatus Mwangiombe Almejiunga na Jumuiya tarehe 3, Mwezi wa Sita tu (June 3, 2014) , ili agombee na hakuwa mwanachama hai kabla ya hapo. Ni Iddi Sandaly na wagombea wengine wawili tu ndio walikuwa wana sifa za kugombea. Lakini tume ilionea kuna haja ya kuwa na uchaguzi wenye kuleta Muamko na Sababu nyingine za Tume. Mgombea Iddi Sandaly hakuwa mchoyo akalikubali hili. Katiba inasema:

ELIGIBILITY
Only paid active members are eligible to run for any office of the Association.  All membership dues shall be paid at least 30 days prior to the election date to be eligible for nomination.  A list of paid financial members shall be made available by the Treasurer for the purpose of election.

Only active members who have resided continuously for a minimum of two years in the METRO, immediately prior to the election date may contest for the office of the president.

Tarehe Ilibadilishwa Tena na tume kwa Sababu ambazo Tume iliziona ni Sababu endelevu kutoka July 31, kwenda August 9.
HARASSMENT ANAYODAI KAFANYIWA LIBERATUS NA VIONGOZI PAMOJA NA ASHA NYANG'ANYI.
Ni kwamba baada ya Liberatus kutoa video ya kampeni ya na kulishambulia Darasa la kiswahili. Asha Nyanganyi kama Mmoja wa Waanzilishi, Msemaji mkuu na Mwalimu wa Darasa la Kiswahili aliwasiliana na Liberatus na Viongozi kwenye email zifuatazo. Naomba mzisome kwa makini. Iddi Sandaly Aliandika response moja TU. Na Ray makamu wa Rais aliandika email mbili Tu. Zote zime ambatanishwa hapa. Hakukuwa na Harassment.

Tunadhani ni kipindi cha Kaka Liberatus Kutambua kwamba DMV kwanza na Aache upotoshaji wa Hali ya Juu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 21, 2014

    kwa kweli kiongozi utamjua kwa maelezo na pointi zake. kwanza ndugu nakupa pongezi kwa kuonyesha ukomavu na nini maana ya kuwa kiongozi. umeonyesha jinsi gani ulivyotumia busara kukubali wengine wagombee ilihali katiba ya jumuiya ilikuwa haiwaruhusu!!!! pili nakupongeza kwa kuweka bayana upotoshaji uliyokuwa kwa makusudi unafanywa na upande wa pili. sasa ukweli tumeujua na hawa wa upande wa pili hawana nia njema na jumuiya yetu. kazi nzuri ya kuweka maelezo sawa. tatu nampongeza mama balozi kwa kazi nzuri ya kuwaita wagombea wote.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 22, 2014

    ACHENI SIASA ZA UDINI, HATA HAMUONI AIBU MNALETA UDINI UISLAM NA UKRISTO MAREKANI..SHAME ON YOU GUYZ.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...