Na Mohammed Mhina, Handeni
Wataalamu wa kilimo wilayani Handeni katika mkoa wa Tanga, kesho watakutana kuweka mezani mapendekezo ya mazao mapya yatakayofaa kwa biashara kwa lengo la kuinua kipato cha mwananchi mmoja mmoja wilayani humo. 
 Mkuu wa wilaya hiyo Bw. Muhingo Rweyemamu, amesema leo kuwa katika mkutano huo, wataalamu hao watapitia itifaki mbalimbali zilizofikiwa na kuanisha zao mbadala kwa biashara kati ya korosho na ufututa ama yote mawili badala ya kutegemea mahindi pekee kwa chakula na biashara. 
 Amesema kwa muda mrefu imebainika kuwa pamoja na kuwa zao la mahindi hulimwa sana wilayani humo, zao ambalo limekuwa halibadilishi hali ya uchumi kwa wakazi wa wilaya hiyo kwa vile zao hilo pia hutumika kwa chakula jambo ambalo amesema kama mwananchi ataamua kuuza kwa upande mwingine hukaribisha baa la njaa katika kaya yake. 
 Amesema kubatikana kwa zao mbadala kutawawezesha wananchi kuondokana na umasikini na wakati huo huo kuendelea kubaki na chakula cha kutosha hadi msimu mwingine wa kilimo tofauti na ilivyo sasa ambapo wananchi walio wengi huuza chakula chote ili kupata mahitaji mengine huku wakibaki bila chakula majumbani hadi kupelekea kuomba msaada serikalini.
Mkuu wa wialya ya Handeni Muhingo Rweyemamu (katikati) akikagua shamba la shule ya sekondari Magamba wilayani humo kuangalia utekelezaji wa maagizo ya kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya iliyotaka kila shule kuwa na shamba darasa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...