Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Mahakama ya Tanzania akibadilishana mawazo na Viongozi wa Tume ya Utumishi wa Mahakama ya Uganda mapema Leo a alipotembelea ofisini kwa Mhe. Jaji Mkuu, wa pili kulia ni Mhe. Jaji James Ogoola, Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Mahakama wa Uganda, wa tatu kulia ni Mhe. Jaji Dk. Esther Kisaakye ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Mahakama ya Uganda, wa kwanza kushoto ni Mhe. Jaji Edward Rutakangwa, Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Tanzania.
Wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Mahakama ya Uganda pamoja na Tanzania wakibadilishana uzoefu jinsi ya kufanya kazi mapema Leo
Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Mahakama ya Tanzania (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe ya Tume ya Utumishi ya Mahakama ya Tanzania na Uganda mapema Leo baada ya kubadilishana uzoefu juu ya utendaji kazi wa Tume hizi. Ujumbe wa Tume ya Utumishi wa Mahakama wa Uganda upo nchini kwa Siku mbili lengo likiwa ni kuja kupata uzoefu jinsi gani Tume ya Utumishi wa Mahakama inafanya kazi. Picha na Mary Gwera, Mahakama ya Tanzania
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...