
Uzinduzi
huo utafanyika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam na tayari wasanii
mbalimbali nchini wameshaalikwa kushiriki.
“Nimekuwa
nikipokea simu nyingi za mashabiki wangu wakitaka nimualike Rebecca, najua kuna
gharama zake kubwa, hivyo kwa kushirikiana na wasaidizi wangu tunalifanyia
kazi.“Napenda
mashabiki wangu wafurahi, lakini pia itategemea ratiba yake naye inasemaje,
hivyo kazi kubwa itafanyika,” alisema Rose.
Rebecca
amewahi kutamba na albamu za Saturday Nite (aliyoitoa Januari 1, 2009), Hlala
Nami (Novemba 11, 2003), Siyabonga (Desemba 21, 2000), Free at Last (Novemba
18, 1997), African Classics (Mei 5, 2009) na Greatest Hits (Januari 10, 2006).
Nyimbo zilizopo katika albamu hiyo mpya ya Muhando ni Bwana Niongoze, Wewe Waweza, Usiniache, Nibariki, Muongo, Kwema, Kamata Pindo la Yesu na Facebook. Hivi sasa Muhando anatamba na albamu yake ya Utamu wa Yesu yenye nyimbo saba, ambazo ni Utamu wa Yesu, Raha Tupu, Tamalaki, Ndivyo Ulivyo, Woga Wako, Imbeni na Kusifu na Achia.
Mbali
na Utamu wa Yesu, Rose Muhando pia amewahi kutamba na albamu za Uwe Macho,
Nyota ya Ajabu (Zawadi ya Krismasi) na Jipange Sawasawa, Kitimutimu, Mungu
Anacheka, Wololo.Pia amepata kung’ara katika wimbo wa Vua Kiatu,
alioshirikiana na Anastazia Mukabwa wa Kenya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...