Mshauri na Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO, Bi. Rose Haji Mwalimu akitoa mada inayohusu mchango wa vyombo vya habari katika kuhamasisha matumizi rafiki ya huduma za kuzuia VVU na Huduma za Afya ya Uzazi kwa Vijana wakati warsha ya siku tatu ya mradi mpya kuhamasisha Vijana kuhusu udhibiti wa Maambukizi mapya ya VVU iliyofanyika hivi karibu katika kituo cha Habari na Mawasiliano Sengerema, Mwanza chini ya mradi wa SHUGA unaoendeshwa kwa pamoja na mashirika ya Umoja wa Mataifa UNICEF na UNESCO kwa kuzishirikisha redio jamii nchini.
Na Mwandishi wetu Sengerema
Licha ya jitihada za serikali na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kupambana na mambukizi ya Virusi Vya Ukimwi hapa nchini, baadhi ya madhehebu ya dini nchini yameelezwa kuchangia kukwamisha juhudi hizo kutokana na imani zao .
Hayo yameelezwa na washiriki wa mafunzo ya siku tatu kwa vyombo vya habari vya jamii Tanzania juu ya kuendesha mradi mpya wa SHUGA unaolenga kutumia vyombo vya habari kutoa elimu na hamasa kwa vijana kukabiliana na maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi.
Washiriki hao kutoka redio mbalimbali za jamii hapa nchini wamesema kuwa kumekuwa na baadhi ya viongozi wa dini ambao kwa namna moja au nyingine hawakubaliani na matumizi ya kondomu kama njia sahihi ya kuzuia sio tu maambukizi ya VVU bali pia magonjwa ya ngono na kama njia ya mpango wa uzazi kutokana na itikadi zao kidini kwa kile wanachokiita kuzuia mimba ni dhambi.
Pichani juu na chini ni Baadhi ya waandishi wa Habari na Mameneja kutoka vituo mbalimbali vya redio za jamii walioshiriki warsha hiyo wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasishwa kwenye warsha hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...