Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania – TRL unawaarifu wananchi kwa jumla kuwa
imefanikiwa kuwasafirisha kuja Dar abiria takriban 678 waliokwama katika Stesheni ya
Manyoni. Zoezi hilo linaloendeshwa kwa awamu mbili tofauti lilianza usiku wa manane
hadi saa 10 usiku wa kuamkia leo .
Kwa mujibu wa taarifa ya uongozi zoezi la pili litaanza tena kuanzia saa asubuhi ya leo
kwa abiria wapatao 699 waliosalia kutegemeana na kupatikana mabasi mengine zaidi ya
11 yanayohitajika.
Kukwama kwa treni hiyo iliyokuwa ikitokea Tabora kuja Dar kumesababishwa na ajali ya
treni ya mzigo iliyokuwa ikienda Bara ambapo ilitokea kati ya Stesheni za Kintinku na
Makotopora km 539/6-0 jana saa 6:50 mchana. Katika ajali hiyo mabehewa 7 yalianguka
na moja liliacha reli.
Tathmini ya Wahandisi wetu ni kuwa kazi ya kukarabati njia itachukua saa 12 na hivyo
njia inatarajiwa kufunguliwa saa 6 usiku wa manane leo.
Safari ya abiria kwenda bara ya leo Julai 08, 2014 itaendelea kama ilivyopangwa hata
hivyo muda wa kuondoka umesogezwa mbele ambapo itaondoka stesheni ya Dar es
Salaam saa 2:30 usiku.
Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Mhandisi
Kipallo Aman Kisamfu.
TRL Makao Makuu,
Dar es Salaam.
Julai 08, 2014
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...