Mbunge wa jimbo la Kilolo Prof. Peter Msola akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mwatasi katika kata ya Bomalang'ombe katika jimbo la Kilolo wilayani Kilolo Mkoani Iringa.
 baadhi ya wakazi wa kijiji cha Mwatasi waliohudhuria mkutano wa hadhara katika kiwanja cha shule ya msingi Mwatasi wakisikiliza hotuba ya mbunge wao Prof Peter Msola
 Mmoja wa wakazi wa jimbo la Kilolo, Ayubu Sanga akitoa taarifa ya kijiji cha Mwatasi mbele ya Mbunge wa jimbo hilo Prof. Peter Msola


 -============ 
Na Denis Mlowe, Kilolo
 
MBUNGE wa jimbo Kilolo, Profesa Peter Msola amewataka wananchi wa jimbo hilo kuwekeza katika elimu kwa kuwapeleka watoto wanaotakiwa kuanza shule na kuondokana na janga la kukosa elimu katika wilaya hiyo.
 
Profesa Msola aliyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Jimbo la Kilolo katika kijiji cha Mwatasi kata ya Bomalang’ombe wakati wa ziara ya siku moja kwa wananchi wa jimbo hilo juzi na kusisitiza umuhimu wa wazazi kuwaelimisha na kuwapatia elimu watoto wao.
 
Msola alisema kuna wazazi ambao wanashindwa kuwekeza katika elimu na kuwafanya watoto wao kukimbilia mijini ambapo maisha ya huko ni magumu bila kuwa na elimu na kuwataka kukazania elimu kwa watoto wao kwanza.
 
Alisema kuwa  maendeleo miongoni mwa jamii yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na kiwango cha uwekezaji katika elimu, ni vema jamii iwekeze kwa kiwango kikubwa katika sekta ya elimu ili kujikwamua na umaskini uliopo na kupambana katika soko la ajira. 

“Tukumbuke kwamba kuwekeza katika elimu ni mkakati wa muda mrefu unaohitaji dhamira, subira na kwamba matokeo yake huonekana baada ya muda mrefu wa uwekezaji na faida kwa wazazi mara baada ya mtoto kusoma na kuweza kumsaidia pindi azeekapo” alisema Prof. Msola
 
Aidha Prof Msola alisema wilaya ya Kilolo ina rasilimali nyingi zinazohitaji viongozi wabunifu watakaohakikisha zinatumiwa vizuri kwa faida ya watu wote hivyo bila kuwekeza katika elimu rasimali hizo zitatumiwa vibaya na watu wasiojua faida ya elimu.
 
Aliongeza kuwa  katika mipango yake ya kuifikisha wilaya hiyo kwenye kilele cha mafanikio, atahakikisha barabara zinazotakiwa kuiunganisha wilaya hiyo na wilaya nyingine zaidi zinajengwa.
 

Alisema hatua hiyo itaongeza shughuli za uwekezaji, utalii, kilimo na biashara na hivyo kuwaongezea kipato wananchi wake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...