Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe, akifurahi na Watoto Yatima na Waishio katika Mazingira Hatarishi wa Kituo cha Nawoda mjini Nachingwea mkoani Lindi kabla ya kufuturu nao futari maalum aliyoiandaa kwa ajili ya watoto hao zaidi ya 80 ambao wanalelewa katika kituo hicho.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (kushoto), akijiandaa kufuturu na Watoto Yatima na Waishio katika Mazingira Hatarishi wa Kituo cha Nawoda mjini Nachingwea mkoani Lindi. Waziri Chikawe aliandaa futari maalum kwa ajili ya watoto hao zaidi ya 80 ambao wanalelewa katika kituo hicho.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (katikati), akizungumza jambo na Shekhe Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Abdul Mpakate (watatu kulia) wakati wa kufuturu futari maalum iliyoandaliwa kwa ajili ya Watoto Yatima na Waishio katika Mazingira Hatarishi wa Kituo cha Nawoda mjini Nachingwea mkoani Lindi. Waziri Chikawe aliandaa futari hiyo kwa watoto zaidi ya 80 wanaolelewa katika kituo hicho.
Shekhe Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Abdul Mpakate akitoa dua la kumshukuru Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (kushoto), kwa kuandaa futari maalum kwa ajili ya Watoto Yatima na Waishio katika Mazingira Hatarishi wa Kituo cha Nawoda mjini Nachingwea mkoani Lindi. Waziri Chikawe aliandaa futari hiyo kwa watoto zaidi ya 80 wanaolelewa katika kituo hicho. Picha zote na Felix Mwagara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...