Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania London unawakaribisha Watanzania wote watakaoweza kupata fursa kuja kuzungumza na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda hapo Ubalozini siku ya Jumamosi (tarehe 12 Julai 2014) kuanzia saa nane mchana hadi kumi na moja jioni (14:00 – 17:00 Hours)

Katika Mkutano huo, Mheshimiwa Pinda anatarajiwa kuzungumzia masuala mbalimbali ya maendeleo ya nchi yetu. Aidha atajibu maswali kutoka kwa washiriki wa Mkutano huo.


IMETOLEWA NA UBALOZI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NCHINI UINGEREZA, LONDON, JUMANNE (8 JULAI 2014)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 09, 2014

    Na hii taarifa tunayosambaziwa kwenye simu ya Kesho Alhamis Reading ni kweli mkutano au kupotezeana muda kama kawaida

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...