Na Rose Masaka
WAZIRI wa Fedha Bi. Saada Mkuya amefanya ziara yake ya kikazi katika Wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam ili  kupata taarifa za makusanyo ya kodi za majengo ikiwa ni eneo moja kati ya maeneo sita ambayo yamepewa kipaumbele katika suala la ukusanyaji wa kodi kama vile eneo la kilimo na miundombinu.
Bi. Saada Mkuya aliahidi kufanya ziara hiyo katika kikao kilichofanyika wiki iliyopita baada ya kurudisha zoezi la ukusanyaji wa kodi za majengo katika Serikali za Mitaa ili kuona kinachoendelea, kupata uhalisia na changamoto zinazowakabili watendaji wote wa Manispaa ya Ilala, Kinondoni naTemeke.
“Tumerudisha makusanyo ya kodi za majengo kwenye mitaa kwasababu ni rahisi na wanajua nyumba zote” alisema Bi. Mkuya.
Kodi ya majengo imekuwa ni moja ya chanzo kikubwa kinachotegemewa na Halmashauri za wilaya zote za Mkoa wa Dar es Salaam. Serikali iliona hili mnamo mwaka 2013 na kuteua chanzo hiki kuwa mfano katika mpango wake wa matokeo Makubwa Sasa (BRN).
Kwa upande wake Mweka hazina wa Wilaya ya Ilala Bw. Stima Kabikile amesema kuwa Halmashauri ya Illala kupitia kitengo chake cha uthamini kwa kushirikiana na viongozi wa kata na mitaa wamejiwekea malengo ya kuyatambua majengo 10,000 ambayo hayakuwepo katika jedwali la awali kwa kutumia njia rahisi ya haraka ya uthamini.
“Tumeweza kubaini na kuongeza idadi ya majengo 6,820 kati ya 10,000 tuliyokadiria yenye thamani ya Shilingi bilioni 989.6 yenye tozo ya kiasi cha shilingi trilioni 1.5 na kuweka kwenye mfumo tayari kwa malipo”. Alisema Bw. kabikile.
Mtaalamu wa kodi za majengo Wilaya ya Ilala Bw. Joseph Kawiche amesema kuwa kila mmiliki wa nyumba hulipa kutokana na asilimia zake ingawa kuna baadhi ya watu ambao hawajaona umuhimu wa suala hili na kuwa wanafichiana majina,kwa hiyo wameona ni vizuri kutumia njia mbadala ya picha ili kuwabaibni wanaokwepa kulipa kodi.
Kwa upande wa Manispaa ya Kinondoni, Mstahiki Meya wa Wilaya hiyo Bw. Yusuph Mwenda amesema kuwa ameona umuhimu mkubwa wa kutumia Serikali za Mitaa na kutoa matangazo kwenye vyombo vya habari na vipaza sauti ili kujenga  uelewa kwa wananchi kuhusu kulipa kodi za majengo.
“Wenyeviti wa mitaa 171,watendaji wa Kata 34 na Watendaji wa Mitaa 171 wanashiriki na kuainisha majengo yaliyoachwa wakati wa uthamini”. Alisema Mwenda.
Mkurugenzi wa wilaya ya Kinondoni Mhandisi Mussa Natty amesema kuwa jumla ya Shilingi bilioni 1.1 zimekwishakusanywa katika majengo 3123,aidha majengo 3120 yaliyobakia yenye wigo wa kodi bilioni 1.4 yao katika hatua nzuri ya ulipaji.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke amesema kuwa Halmashauri imekusanya kiasi cha shilingi milioni 165.7 kutokana na majengo ambayo awali hayakuwepo katika daftari la majengo ambapo mapato yanatarajiwa kuongezeka kwa hali ya juu katika mwaka huu wa fedha baada ya majengo yote 10,000 kuthaminiwa.
Baadhi ya changamoto zinazozikabili Wilaya hizo ni pamoja na waraka wa msamaha wa kulipa kodi ya majengo wakati sheria ipo kimya wakati wanamiliki majengo ya makazi,kupangishana biashara  ambao raia na wanajeshi wastaafu wanao,pia shule binafsi kudai kutoa huduma wakati ada zao zipo juu, hivyo Manispaa zote tatu zimetoa wito kwa wananchi wa Tanzania kulipa kodi kwa hiari na Serikali iweke wazi sheria za misamaha kama zipo.
 Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya (kulia) Ilala akimsomea taarifa ya makusanyo ya kodi za majengo na mikakati  yake ya kufikia malengo waliojipangia ili kuongeza mapato Mhe. Waziri wa Fedha Bi. Saada Mkuya wakati wa ziara ya siku moja katika Manispaa za Ilala, Temeke na Kinondoni.
 Waziri wa Fedha, Mhe. Saada Mkuya akipitia moja ya taarifa alizopewa na uongozi wa Halmashauri wilaya ya Kiondoni wakati alipofanya ziara yake ya siku moja ofisi hapo.
 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Bw. Yusuph Mwenda (kulia) akitoa maelezo yake kwa Waziri wa Fedha, Mhe. Saada Mkuya (kushoto) wakati wa mkutano na viongzoi wa Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha, Mhe. Saada Mkuya akitoa hotuba fupi yenye kuwaelekeza viongzoi wa Manispaa ya Temeke huku akiwasisitizia kutumia mifumo ya TEHAMA katika kuleta ufanisi ukusanyaji kodi kama njia rahisi inayowasaidia walipaji kodi kutopata usumbufu wakati wa ulipaji. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...