Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhe. Christopher Chiza(Shati jeupe) akiangalia zao la Mahindi yaliyolimwa katika Bustani Maalum ya Shamba Darasa katika Banda la Jeshi la Magereza alipotembelea Banda hilo kujionea Kilimo cha Kisasa na Biashara Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa, Jijini Dar es Salaam(wa kwanza kulia) ni Mtaalam wa Kilimo wa Jeshi la Magereza, Mrakibu wa Magereza, Uswege Mwakahesya.
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhe. Christopher Chiza akiangalia zao la Kitunguu kinachozalishwa na Jeshi la Magereza katika Gereza Mang'ola Mkoani Arusha alipotembelea Banda la Jeshi la Magereza, Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa, Jijini Dar es Salaam. Mhe. Waziri Chiza ameahidi kushirikiana na Jeshi la Magereza katika kutafuta fursa ya Masoko ya ndani na nje ya nchi(wa pili kulia ni Afisa Masoko wa Shirika la Magereza, Mrakibu Msaidizi wa Magereza, Yunge Saganda.
Muonekano wa Bustani ya Shamba Darasa katika Banda la Jeshi la Magereza lililopo katika Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ambapo sehemu kubwa ya Wananchi wananufaika na Elimu ya Kilimo cha Kisasa na chenye tija katika Maonesho hayo yanayoendelea Jijini, Dar es Salaam.
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhe. Christopher Chiza(Shati jeupe) akifanya mahojiano na Mwandishi wa Habari baada ya kutembelea Bustani Maalum ya Shamba Darasa ya Jeshi la Magereza iliyopo katika Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa, Jijini Dar es Salaam. Katika Mahojiano hayo Mhe. Waziri ameahidi Kushirikiana na Jeshi la Magereza katika kutoa elimu ya Kilimo Bora kwa Wakulima hapa Nchini pamoja na kulisaidia Jeshi hilo ili kupata fursa mbalimbali ya kupata Wawekezaji wa ndani na nje ya nchi katika masuala ya Kilimo.
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhe. Christopher Chiza akiondoka katika Banda la Jeshi la Magereza alipotembelea Banda hilo Julai 7, 2014 katika Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Jijini, Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 08, 2014

    Kilimo ndiyo uti wa mgongo wa taifa hili, kinasitiri watanzania wengi kwa upande wa lishe na kipato. Tukiboreshe kwa kulima mashamba makubwa na madogo ili kiweze kuendelea kutusitiri.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...