Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel inayotoa huduma nafuu na yenye wigo mpana zaidi wa mawasiliano, imeshirikiana na mbunifu wa mitindo Afrika ,Mustafa Hasanali katika kusheherekea miaka 15 ya mafanikio yake makubwa katika sekta ya mitindo.
Mustafa Hassanali amefanya maonyesho katika miji 27 katika nchi 18, na kugusa maisha ya watu mbali mbali kwa njia tofauti. Na anaendelea kuwa maarufu katika sekta ya mitindo nchini na Afrika kwa ujumla.
Ushirikiano huo kati ya Airtel na Guru wa mitindo Tanzania na nje ya Tanzania, utawezesha wateja wa Airtel na washabiki wa mitindo kuwa karibu zaidi na ulimwengu wa mitindo kwa kupata habari mbali mbali na za kisasa kupitia simu zao za mikononi.
Akiongea kuhusu muungano huo Mkurugenzi wa huduma kwa wateja wa Airtel Tanzania Adriana Lyamba, alisema “mitindo ni moja kati ya vipengele muhimu katika maisha yetu, zikiwemo nguo, vifaa na vyombo mbalimbali.
Kila mtu anataka kupendeza na kujihusisha na mitindo ya kisasa. Ila , hivi sasa upatikanaji wa habari na huduma za mitindo ni mgumu sana. Hivyo Airtel tumekuwa wa kwanza katika kuwapatia wananchi huduma hii kupitia simu zao za mkononi itakayowasaidia kupata habari mbali mbali za mitindo kwa ujumla . Huduma hii inajulikana kwa jina la “Airtel Fasheni”.
Tunaamini kuwa , huduma hii itawasaidia wateja wetu wote ambao wangependa kupata habari mbali mbali na kuwafikia wabunifu wa mitindo ili kupata ushauri na pia kununua bidhaa zao.”
Mustafa Hassanali, mbunifu mitindo mahiri Afrika alisema , “ Airtel fasheni ni huduma ya kipekee ambayo wateja wa Airtel wanaweza kuipata mahali popote na wakatii wowote kwa kupiga *148*82#. Huduma hii ni Tsh.90 kwa siku.”
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...