Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewashauri albino wanaoishi Jijini Dar es Salaam kuwa karibu sana na Jeshi hilo ili kurahisisha mawasiliano kati yao na Wakuu wa vituo vya Polisi vilivyo karibu na makazi yao au wanapofanyia usalama wao jijini Dar es Salaam.

Pamoja na kwamba haijawahi kutoa tukio lolote dhidi ya Albino jijini Dar es Salaam kutokana na uhusiano uliopo lakini kwa sasa waongeze mawasiliano na Jeshi la Polisi kutokana na taarifa za uhalifu dhidi ya Albino katika baadhi ya mikoa hapa nchini.

Pia Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam SULEIMAN KOVA ameongea na Albino hao ofisini kwake na kuwaambia kwamba Jeshi la Polisi kwa ujumla linaendelea na jitihada kubwa sana kupambana na maadui wa Albino ambao ni wahalifu na wengi wao wameishakamatwa na kufikishwa mahakamani ambapo wengine wameishahukumiwa.

Albino wanatakiwa kuonyesha ushirikiano wa hali ya juu na Jeshi la Polisi hata kama hakuna tishio la aina yoyote wanalolijua katika maeneo yao ya makazi au wanapofanya shughuli zao za kikazi.

Katika kufanikisha zoezi hilo la mawasiliano ya haraka na Jeshi la Polisi, Kamishna wa Polisi Kanda Malum ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na wadau kampuni ya SAPNA ELECTRONIC ametoa simu 20 kwa Albino ambao wameudhuria kikao ili iwe rahisi kwao kuwasiliana Jeshi la Polisi kwa namba 0787-668306 ambayo ipo katika chumba cha dharura katika Kikosi cha 999.

Kamishna Kova anaendelea kuongea na wadau mbali mbali ili misaada zaidi ipatikane kwa walemavu wa ngozi ambao ni Albino ili waweze kupata simu za mikononi, mafuta maalum ya kupaka ngozi zao na msaada mwingine wowote ambao utafaa kwa Albino hao kupitia kwa namba 0715 – 009983 hii ni namba ya Kamishna mwenyewe ya oisi na namba nyingine ya Msaidizi wake katika suala la kuwasaidia Albino ni 0756-710179 ambayo ni ya SP. MOSES NECKEMIAH FUNDI.

Aidha zipo jitihada za makusudi zinazofanyika kati ya Polisi Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam na uongozi wa Mkoa na Kitaifa kwa manufaaa ya ulinzi na Usalama wa Albino wote.

Hatua zingine za ziada za muda mfupi na mrefu ni uwepo wa program ya mafunzo maalum kwa Albino wa Jijini Dar es Salaam ili wapate mafunzo kupitia dhana ya Polisi Jamii na Ulinzi Shirikishi kwa lengo la kupata uelewa wwa kutosha ili nao pia washiriki na kujua namna ya kutoa taarifa kwa lengo la kujikinga na maadui wao ambao wamegubikwa na tama za kujipatia mali, madaraka n.k. kwa njia za ushirikina.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Napata taabu sana kuelewa uwezo wa hili jeshi letu ktk kulinda raia hasa hawa wahanga wa hili suala.....ivi kweli tunahitaji advanced sophisticated methods kuwatambua wahusika wa uharamia huu??? naamini ugumu wa kumpata adui yategemea na mbinu za huyo adui kujificha dhidi ya mkono wa sheria...sasa ni kweli hawa wamezidi mbinu za kiintelijinsia za kipolisi??Nasema tena hapa hili suala likishikwa kwa mikono miwili na wenzetu na likishapata nguvu ya kimtandao litatukwamisha ktk kiwango cha kitaifa na kimataifa....Binafsi nilishagharimika kwa kukimbiwa na mchumba wangu wa kizungu 2011 nilipokua East Europe...baada ya kuona taarifa za mauaji yeye alifikiri ni yanahusisha hata weupe kama yeye......sasa hizi ni individual payback...tusubiri gharama za kitaifa na kimataifa ndio tutatia akili...inauma sana jamani.....

    ReplyDelete
  2. Nimeona ile nyumba yule mama aliyekatwa mkono na mume wake kuuawa siyo nzuri kabisa, wengine wamependekeza aamie mjini lakini hawakueleza ataaishije huko. Wazo langu ni kuhamasisha wananchi wenzangu tuanze kwa kuchangia makazi ya huyu mama atakaporudi akute nyumba ya maana na angalau kipato cha kujikimu kwa mwaka mmoja, kama chama cha maalbino kinakubaliana michango ya hiari ichangishwe kupitia simu au njia nyingine.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...