BAADA ya timu ya taifa ya vijana ya Tanzania chini ya miaka 17, Serengeti Boys kutolewa katika michezo ya kuwania kufuzu fainali za Afrika za vijana na Afrika kusini kwa wastani wa mabao 4-0, Rais wa shirikisho la soka Tanzania, TFF, Jamal Emil Malinzi amekiri kuwa bado timu haijaandaliwa vizuri.

Rais Malinzi amesema tatizo la timu ni maandalizi yasiyoridhisha yanayochangiwa na kukosa mfumo sahihi na mpango mzuri wa soka la vijana.

“Tatizo letu ni lile lile, kwenye maandalizi, lakini tunapozungumzia maandalizi tunazungumzia uwezo wa kiuchumi, kwamba timu yetu inaandaliwaje,” Alisema Malinzi.

“Tunaweza kusema timu imejitahidi, Lakini kiukweli hii ndio mechi yao ya pili ya kimataifa, mechi yao ya kwanza walicheza na Afrika kusini nyumbani.

“ Kwahiyo lazima sisi tukae kama nchi, kama shirikisho ili tuweze kuangalia programu zetu za soka la vijana ili watoto kama hawa kabla hawajaingia katika mechi kama hizi wawe wameshakaa kama timu kuanzia umri wa 12, 13, 14 na 15 , yaani wakae miaka minne kwenye timu ya taifa,” Aliongeza Malinzi.

Aidha, Rais Malinzi alisema shirikisho hilo limejipanga upya ili kuhakikisha nchi inakuwa na mfumo sahihi wa soka la vijana. “Kipo ambacho kinafanyika, tunaandaa mpango wa kitaifa wa maendeleo ya soka la vijana na tutazindua mwezi wa 10 mwaka huu, siku ambayo TFF itatimiza miaka 10 ya kujiunga na FIFA na tutaeleza haya tunayoyasema ili kama nchi tuwe na mpango endelevu wa soka la vijana,”

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. The mdudu,yaleyale yaani hatuna jipya kabisa huu uongozi umeingia madarakani kwa mbwe mbwe kubwa sn na ahadi lukuki sasa mm najiuliza hivi kwanini mlipeleka timu? Huku mkijua kabisa timu haina maandalizi yoyote ya maana,,hivi huu ujinga utaisha lini? Kwenye mashindano ya komoniwosi mlipeleka wanamichezo zaidi ya 30 lakini wamekuja kututia aibu na kama mnavyonijua The mdudu mie kwa uzalendo mbele ya Taifa langu la TZ nimeingia kwa makile ya hali ya juu kabisa najibendera langu kubwa la TZ huku nikilipepelusha bira ya woga..kumbe mmh wale wanamichezo wetu wote ni mizigo isiyobebeka kabisa tena nilibahatika kuongea na mabondia nakuwatoa woga kwamba mko ugenini msitegemee sn hawa waamuzi dawa yao ni nyie kumdondosha mpinzani wako kwenye sakafu kwa makonde mazito mazito lakini wapi imeniuma sn moyoni,wakimbiaji na ndio hivyo tena hoi bini taabani,,wamenifanya mpaka nichukue uwamuzi mgumu wa kukunja BENDERA YANGU TAKATIFU na kujiludia nyumbani kulikoni kuumia zaidi moyoni..ndugu zanguni watanzania lazima tubadilikeni mafanikio hayaji bila ya maandalizi ya ukweli na nia pia toka moyoni mwako na wala sivinginevyo PENYE MAFANIKIO PANA MAANDALI.hata kwa madada zetu wanalijua hili huwezi pika chakula kizuri pasipo na maandalizi mazuri ya vitu vyote unavyohitaji kwenye hayo mapishi yako.

    ReplyDelete
  2. Anzisheni somo la soccer mashuleni na vyuoni ili vijana wasomee tangu wakiwa wadogo kama wenzetu wafanyavyo huku nje.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...