Wananchi wameendelea kutahadharishwa kuwa macho na tabia ya baadhi ya wanasiasa wenye hulka ya kushawishi jamii kutoshiriki harakati za maendeleo na ustawi wa jamii kwenye maeneo yao kwa sababu tu ya itikadi ya kisiasa.

Tahadhari hiyo imetolewa na Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi wakati akikabidhi vifaa mbali mbali vya uwezekaji wa majengo ya Maabara na Maktaba ya Skuli ya Sekondari ya Fujoni iliyomo ndani ya Jimbo la Kitope Wilaya ya Kaskazini “ B”.

Balozi Seif ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema ipo miradi mingi ya maendeleo ya wananchi katika maeneo tofauti mengine ikipata usaidizi wa ufadhili wa wawekezaji waliomo katika maeneo hayo, lakini cha kushangaza ni kuona baadhi ya wanasiasa walafi hushawishi wananchi hao wasijihusishe kushiriki katika miradi hiyo.

Balozi Seif aliushukuru na kuupongeza Uongozi mzima wa Kamati ya Skuli ya sekondari ya Fujoni kwa umahiri wake wa kuwajengea hatma njema ya kielimu watoto wao.

Mapema Mke wa Mbunge wa Jimbo la Kitope Mama Asha Suleiman Iddi lielezea masikitiko yake na kulaani kitendo kilichofanywa na baadhi ya watu kumsingiziwa kwamba aliahidi kujenga madrasa moja iliyomo ndani ya Kijiji cha Fujoni jambo ambalo niuzushi unaotaka kumuharibia kisiasa.

Alieleza kwamba tabia aliyojijengea ndani ya jamii ni kwamba anapo ahidi jambo tayari ameshajiandaa na kamwe hachukui muda mrefu kuitekeleza ahadi hiyo akielewa kwamba asipotekeleza tayari ameshabeba dhima kwa mwenyezi mungu.

Akitoa shukrani kwa niaba ya Uongozi wa Kamati ya Skuli Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Sekondari ya Fujon i Mwalimu Mbrouk Ishaq Daima alimuhakikishia Mbunge huyo wa Jimbo la Kitope kwamba Kamati hiyo itakuwa tayari wakati wote kutekeleza malengo yanayopangwa katika skuli hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seiof Ali Iddi akibadilishana mawazo na Uongozi wa Kamati ya Skuli ya Sekondari ya Fujoni mara baada ya kukaguwa majengo ya Maabara na Maktaba na kukabidhi mbao kwa ajili ya uwezekaji majengo hayo.
Balozi Seif akimkabidhi Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Sekondari ya Fujoni kulia yake Maalim Mabrouk Ishaq Daima Mbao pamoja na mitwiko yake kwa ajili ya uwezekaji majengo mapya ya Maktaba na Maabara ya Skuli hiyo.
Balozi Seif akikabidhi Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Fujoni Maalim Mabrouk Ishaq Daima fedha za fundi wa uwezekaji wa mapaa ya majengo ya Maabara na Maktaba ya Skuli hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif akizungumza na Uongozi wa Kamati ya Skuli ya Sekondari ya Fujoni ndani ya Ofisi ya Mwalimu Mkuu mara baada ya kukabidhi vifaa kwa ajili ya uwezekaji wa majengo ya Maabara na Maktaba ya Skuli hiyo. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...