Baraza la madiwani la halimashauri ya wilaya ya chato katika kikao chake robo ya nne,
limetunuku vyeti, ngao na pesa Taslimu ikiwa ni pongezi kwa shule na kata zilizofanya
vizuri katika mtihani wa darasa la saba 2014.
Shule binafsi zilizoongoza ni shule ya msingi Kadama (Kadama English medium),
ikifuatiwa na shule ya msingi Emau ( Emau english medium) zote zipo wilayani Chato.
Shule za serikali zilizoongoza ni shule ya msingi Magiri iliyoshika nafasi ya kwanza,
nafasi ya pili ilimeshikwa na shule ya msingi Minkoto “A”, na kufuatiwa na shule ya
msingi Imalabupina iliyoshika nafasi ya tatu, huku shule ya msingi Kamanga iliyopo kata
ya Makurugusi ikishika nafasi ya mwisho na kukabidhiwa kinyago.
Kata zilizofanya vizuri katika tuzo hizo ni pamoja na Kasenga, Muganza na Buziku.
Katika hatua nyingine Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Chato
limewatunuku vyeti vya pongezi wananchi wawili wa kata ya Nyamirembe Ndg.
Rajabu Athumani Ndugala na Abdu Ibrahimu Mpisi ambao walifanikisha ujenzi wa
madarasa mawili na ofisi ya mwalimu shule ya msingi Nyamirembe B kwa gharama ya
Tshs.16,000,000, huku halmashauri ya Wilaya ya chato ikikamilisha madarasa na fisi
hizo kwa kwa thamani ya Tshs.15,000,000.
Afisa elimu wa wilaya ya Chato Bw. Angasirini Obedi Kweka akitoa maelezo kwa
baraza la Madiwani kabla ya kukabidhi tuzo hizo alisema, Ufauru mzuri wa wanafunzi
huchangiwa na uwepo wa walimu wakutosha na wenye kuwajibika, chakula kwa
wanafunzi wawapo shuleni na ushirikiano baina ya wanajamii.
Bw. Kweka aliendelea kuelezea changamoto zilizopo mashuleni, hususa ni madawati
ambayo yamekuwa changamoto kubwa hasa shule za msingi ambapo alisema idadi
ya wanafunzi inazidi kuwa kubwa ukilinganisha na idadi ya madawati yaliyopo , hivyo
aliliomba baraza la madiwani kulifanyia kazi tatizo hil.la
bi. Leticia Pastory wa Kadama English medium akipokea ngao na cheti
kwa kuwa mshindi wa kwanza katika mtihani wa darasa la saba wilayani Chato.
bw Edward Leornad mratibu wa elimu kata ya Kasenga akipokea cheti
cha kata ya kwanza kiwilaya katika mtihani wa darasa la saba 2013.
Bw. Lucas Nicholaus mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Kamanga
shule iliyokuwa ya mwisho katika mtihani wa darasa la saba 2013 akipokea kinyago,
ambacho hukabidhiwa kwa shule inayofanya vibaya kila mwaka.
baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Chato katika
kikao cha robo ya nne.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...