Naibu Mtendaji Mkuu, Ofisi ya Rais-Usimamizi wa Utekelezaji wa Miradi (Presidents Delivery Bureau - PDB) inayosimamia Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now! - BRN), Bw. Peniel Lyimo, akifungua semina ya siku nne, ya tathmini ya Utekelezaji wa BRN kwa Mwaka wa kwanza; inayohusisha watendaji kutoka wizara na sekta mbalimbali zinazotekeleza BRN. Semina hiyo imefunguliwa leo Jumatatu jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya washiriki wakifuatilia mada katika semina hiyo ya tathmini inayohusisha watendaji wa BRN iliyofunguliwa jijini Dar es Salaam leo Jumatatu. Semina hiyo inayowakutanisha watendaji wapya wa PDB na BRN pia inahudhuriwa na maofisa wanahohusika na utekelezaji katika ngazi ya Wizara, Taasisi na Mikoa.
Watendaji kutoka Ofisi ya Rais-Usimamizi wa Utekelezaji wa Miradi (PDB) wakijadiliana jambo wakati wa semina ya tathmini inayohusisha watendaji wa BRN iliyofunguliwa jijini Dar es Salaam leo Jumatatu. Kutoka kushoto ni Meneja Mawasiliano na Utetezi, Bw. Hassan Abbasi, Mkurugenzi wa Huduma za Utawala wa PDB, Bw. Maharage Chande na mtaalamu wa PDB kutoka PEMANDU Malaysia, Bw. Marc Shien Loong.
Naibu Mtendaji Mkuu wa PDB, Bw. Peniel Lyimo (kulia) akijadiliana jambo na baadhi ya watendaji wake wanaosimamia sekta ya kilimo katika BRN. Kutoka kushoto ni James Ngwira kutoka PDB, Bw. January Kayumbe Mkuu wa Kitengo cha Utekelezaji wa BRN katika Wizara ya Kilimo na Bw. Henry Kinyua, Mkurugenzi wa Idara ya Kilimo - PDB.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...