Idara ya Uhamiaji nchini  imewakamata raia wanane  wa kigeni  (pichani chini) wakati wakiingia nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu  Nyerere wakiwa na pasipoti bandia za kusafiria za Mataifa tofauti ya Ulaya. 
Wageni hao walikuwa wakijaribu kuingia nchini leo tarehe 15.08.2014 majira ya saa nane na nusu usiku kwa ndege ya shirika la ndege la Uturuki yenye Namba TK 603,  wakitokea Uturuki na kujitambulisha kuwa ni raia wa Sweden na Belgium. 
   Maofisa Uhamiaji katika kituo hicho baada ya kuwatilia mashaka na kuwafanyia ukaguzi wa kina, waligundua kuwa wageni hao ni Raia wa Iraq wakijaribu kuingia nchini Tanzania na pasipoti za bandia.       
Kukamatwa kwa wageni hao ni jitihada za Idara ya Uhamiaji kupambana na Uhamiaji haramu nchini ambapo suala la zima la udhibiti wa mipaka linapewa kipaumbele. 
Akizungumzia tukio hilo, Kaimu Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Tatu Burhan, anasema, kwa kutumia ujuzi na weledi walionao Maofisa Uhamiaji wanaendelea kufanyakazi usiku na machana kuhakikisha Sheria na Taratibu za Uhamiaji zinafuatwa.
 "Idara ya Uhamiaji, iko macho hatulali ili kuhakikisha ulinzi na usalama wa nchi ikiwa ndio jukumu letu namba moja unaimarika. kwahivyo, kila mtu awe raia wa kigeni na Watanzania wanapaswa kufuata Sheria na Taratibu zilizopo za kuingia na kutoka nchini"
   Hadi sasa, Wageni hao wamezuiliwa kuingia nchini na wanaendelea kushikiliwa na Maofisa wa Idara ya Uhamiaji kituoni hapo huku wakisubiri kurudishwa walikotoka.  
Hili ni wimbi lilioibuika hivi karibuni kwa baadhi ya raia wa nchi za Iraq, Iran, Syria kujaribu kuingia nchini isivyo halali huku ikisemekana lengo lao kubwa ni kuingia Tanzania na baadae kutoka kuelekea mataifa ya Ulaya.
 Majina ya Wageni hao na Pasipoti bandia walizokuwa wakitumia pamoja na Majina halisi na Pasipoti zao za Iraq zilizogunduliwa baada ya upekuzi kwenye mabano ni kama ifuatavyo;
  
1. ADEL SHAALAN MOHAN - SWEDISH, PPT. NO. EI282207 ( ADEL SHAALAN MOHAN Pasipoti Nam. G1489664)
2. SAMER HELMI KAMIT    -  SWEDISH, PPT. NO. 87187804 ( LAZIM MOSA HITEET, PPT. Namba, A 13466001)
3. MOHAMMED JAFAR AL MOSAWI - SWEDISH, PPT.NO. 87168871 (ALI HUSSEIN OLEIWI, PPT. NO. G 1111623)
4. DAVID GABRIEL POBLETE    - SWEDISH PPT.NO. 86867751 (AYAD SAMI MAKTTOOF, PPT NO. A 4910203)
5. SADDAM ALKHAMERI AREF   - SWEDISH, PPT NO. 81640513 (SAIF ALDAN FALIH HASAN, PPT. NO. G 1489664)
6. ALI MOHAMMED ABDULLAH - IRAQ, PPT. NO. A 5931725
7. OSAMAH ZAID GHAEB AL-OBAIDI    - IRAQ, PPT. NO. A 6175951
8. ALI HUSSEIN OLEIWI      - IRAQ, PPT. NO. G 1111623 




    

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Uhamiaji endeleza kazi hizi ili mchangie ulinzi wa mipaka ya nchi hii kama mnavyotarajiwa kufanya.

    ReplyDelete
  2. wahusika wa uhamiaji swala la wahamiaji wanaotokea nchi zenye hali ya machafuko ya usalama kama Gaza-Palestine na Iraq ni swala la kimataifa tusiwachukulie wote
    kama wahamiaji haramu yawezekana
    umoja wa taifa umechangia kuwasaidia vyeti vya usafiri walivyonavyo kutokana na hali halisi ya mauaji yasiyo na msingi zidi ya tofauti za dini na siasa.
    Tanzania chini ya uongozi wa awamu ya kwanza baba wa Taifa na serikali walifanya maamuzi magumu ya kuwapatia hati za usafiri za Tanzania viongozi wa Frelimo na South Africa kumbukumbu rudieni
    hotuba ya raisi Jakaya Kikwete akiwepo South Africa kuhusu matumizi ya hati za Tanzania kwa raisi mstahafu Tabu Mbeki na wengine.Tanzania tuendelee kuwa wavumilivu na wahamiaji wa nchi zenye machafuko.Palestine na Iraq ni marafiki zetu sawa wachina na wahindi.wapewe ushauri,misaada ya kimataifa kama hawana nia mbaya.
    MIKIDADI-DENMARK

    ReplyDelete
  3. Great work by Immiigration really deserve the credits to intercept and cupture those Illegals because who knows as to why they were trying to inter the country with false identity? But the great job doesn't end there. They should continue to dig deeper to find out the really identity of those 8 illegals and the reason why they ware trying to infiltrate our country. They could be Terorrists

    ReplyDelete
  4. Kwanini Tanzania????Je yawezekana kuna wenzao waliofanikiwa awali??Ni dhahiri si mpango mdogo.......tuwe macho zaidi si hapo tu.....huko mipakani ndio usiseme......kwakua hatutumii satelite wa...........

    ReplyDelete
  5. Huenda wana uraia wa kupewa toka Sweden sababu ya ukimbizi na wamekuja tafuta uwekezaji bongo,pale sweden wanawapa hao uraia Sababu kwao kuna vita

    ReplyDelete
  6. Hata kama nchi zao zina hali ngumu suala Zima linabakia kuwa KWA NINI WAGUSHI NYARAKA!!!? Ni bora wangejisalimisha kama wakimbizi basi halafu uhamiaji ijue cha kufanya.

    Hivi vitambulisho vya taifa viko wapi jamani? Haiwezekani waje hivi hivi, ina maana kuna wenzao tayari wameshafanikiwa kuingia kilaini. Msako mkali ufanyike kuwabaini ambao tayari wamo nchini.

    ReplyDelete
  7. Ni kazi nzuri na ya kuonyesha umakini kwa idara ya Uhamiaji.

    Lakini wote tumesahau kuwa hawa raia pengine wana uraia wa nchi mbili na walitaka kwenda mahala.

    Uchunguzi uwe ni kubaini kama wana uraia pacha na lini kusudio la safari yao.

    ReplyDelete
  8. Iraq inarusu uraia wa nchi mbili. Hivyo kuwa na passport zao za asili, isiwe sababu ya kuwa wahamiaji haramu.

    ReplyDelete
  9. Watatuletea vita.Warudisheni kwao

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...