Rais Jakaya Mrisho Kikwete,
Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali, Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda,
Waziri wa Sheria na Katiba Dkt Asha-Rose
Migiro, Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Zanzibar
Mhe Omar Othman Makungu, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, Mwanasheria Mkuu Jaji Frederick Werema, Mtendaji Mkuu wa Mahakama Mhe Hussein kattanga katika picha ya pamoja na
Majaji wa Mahakama kuu ya Tanzania baada ya kuapishwa leo Ikulu jijini Dar es
salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Omar Othman Makungu pamoja na Majaji wa Mahakama ya Rufaa Tanzania na Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania wapya
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Omar Othman Makungu pamoja na Majaji wa Mahakama ya Kuu Tanzania na Majaji wapya
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Omar Othman Makungu pamoja na majaji wapya
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Omar Othman Makungu na Jaji Kiongozi Shaban Ally Lila wakiwa na Majaji wapya
Rais Kikwete na Waziri wa Sheria na Katiba Dkt Asha Rose Migiro wakiwa wa wanachama wa Chama cha Wanasheria Wanawake (TAWLA) na Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania wanawake wapya
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Omar Othman Makungu na Jaji Kiongozi Shaban Ally Lila wakiwa katika pic ha ya jumla na Majaji wapya na wa zamani. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete asubuhi ya
leo, Ijumaa, Agosti 15, 2014, amewaapisha Majaji 20 wapya wa Mahakama Kuu ya
Tanzania ambao aliwateua mwanzoni mwa wiki hii katika hafla iliyofanyika Ikulu,
Dar Es Salaam.
Halfa
hiyo iliyofanyika Ikulu, Dar Es Salaam ilihudhuriwa pia na Makamu wa Rais
Mheshimiwa Mohamed Gharib Bilal, Waziri
Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda, Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande
Othman, Waziri wa Katiba na Sheria Mheshimiwa Asha Rose Migiro na Jaji Mkuu wa
Zanzibar Mheshimiwa Omar Othman Makungu.
Majaji
hao wapya wa Mahakama Kuu ya Tanzania ni pamoja na akinamana wanane na uteuzi
huo wa Mheshimiwa Rais Kikwete umeshirikisha wanasheria kutoka Serikalini,
Taasisi za Umma, Jumuia ya Afrika Mashariki, Sekta Binafsi na Asasi za Kiraia.
Majaji
hao wapya ambao wameapishwa leo ni Jaji Penterine Muliisa Kente, Jaji Benedict
Batholomew Mwingwa, Jaji Eliezer Mbuki Feleshi, Jaji John Eudes
Ruhangisa, Jaji Winfrida Beatrice Korosso, Jaji Lilian Leonard Mashaka, Jaji
David Eliad Mrango, Jaji Edson James Mkasimongwa, Jaji Mohamed Rashid Gwae na
Jaji Firmin Nyanda Matogoro.
Wengine
ni Jaji Leila Edith Mgonya, Jaji Barke Mbaraka Abdou Sehel, Jaji Awadhi
Mohamed, Jaji Lugano J. Mwandambo, Jaji Rose Ally Ibrahim, Jaji Paul Kihwelu,
Jaji Modesta Opiyo Makopolo, Jaji Amour Said Khamisi, Jaji Mary Caroline Levira
na Jaji Salma Maghimbi.
Imetolewa
na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
15
Agosti, 2014
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...