KIKUNDI cha Ngoma za asili cha Bujora cha jijini Mwanza kimefanikiwa
kuchukua ubingwa wa fainali za mashindano ya Ngoma za asili kanda
ya ziwa mwishoni mwa wiki kwa pointi 87.5 zilizofanyika katika Uwanja
wa Mabatini kwa kushirikisha mabingwa wawili kutoa katika mikoa
mitano ambayo ni Tabora, Shinyanga, Kagera,Mara na Mwanza.
Kwa ubingwa huo kikundi cha Bujora kilizawadiwa pesa taslimu shilingi
1,100,000/= , kikombe pamoja na medali za dhahabui cha Mwanalyaku
ambao walipata pointi .
Nafasi ya Pili katika fainali hizo ilichukuliwa na kikund Mwanalyaku cha
jijini Mwanza pia kwa pointi 79.5 na hivyo kuzawadiwa pesa taslimu
shilingi 850,000/=,
Nafasi ya tatu ilichukuliwa na kikundi cha Bugoloile cha Kagera kwa
pointi 79.3 na hivyo kuzawadiwa pesa taslimu Shilingi 600,000/=.Nafasi
ya nne ilikwenda kwa kikundi cha Mabulo ya Jeshi cha Sinyanga kwa
pointi 76.7 na hivyo kuzawadiwa pesa taslimu Shilingi 500,000/=.
Nafasi ya tano mpaka ya kumi ni kikundi cha Rugu kagera pointi
75.2,Musoma One cha Mara 73.8,Wanunguli Shinyanga pointi
73.1,Magereza Tabora 70.1,Kiwajaki Mara 69.6 na cha mwisho ni
kikundi cha Bugobogobo cha Tabora pointi 59.3.
Mgeni rasmi katika fainali hizo alikuwa Kaimu Kamanda wa Polisi wa
Mkoa wa Mwanza, Christopher Fuime ambaye aliishukuru Kampuni ya
Bia Tanzania kwa kuzamini mashindano ya ngoma ambayo hufanyika
kila mwaka wakati wa mavuno ambapo aliwaomba waendelee
kudhamini kwani yanatukumbusha asili yetu tulikotoka na pia zawadi
wanazopata zinaongeza kipatao kwa washiriki.
Nae Meneja wa Bia ya Balimi Extra Lager, Edithi Bebwa aliwashukuru
washiriki wote kwa kuwa mabingwa wa mkoa yao huko wanakotoka na
pia aliwashukuru kwa kushiriki fainali za Kanda na kuwaahidi kuboresha
zaidi mashindano mwaka ujao hasa upande wa zawadi.
Edithi alisema sababu msinigi ya kuwepo kwa Mashindano ya Balimi
Ngoma za Asili ni kuenzi na kulinda utamaduni wa Kitanzania.
Kampuni ya Bia nchini ni sehemu yao ya kurudisha fadhila kwa
watumiaji wa Kinywaji cha Balimi Extra Lager pamoja na vinywaji vyote
vya Kampuni ya Bia Tanzania(TBL).
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Christopher Fuime(kulia) akimkabidhi kikombe kiongozi wa kikundi cha ngoma cha Bujora mara baada ya kuibuka mabingwa wa Kanda ya Ziwa wa fainali za mashindano ya Ngoma za Asili yalifanyika katika Uwanja wa Mabatini jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya wacheza ngoma wa kikundi cha Bujora wakishangilia na kikombe pamoja na pesa taslimu shilingi 1,100,000/= mara baada ya kuibuka mabingwa wa Kanda ya Ziwa wa fainali za mashindano ya Ngoma za Asili yalifanyika katika Uwanja wa Mabatini jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...