Mcheza sinema na mchekeshaji maarufu duniani aliyepata kushinda tuzo ya Oscar Robin Williams amefariki dunia katika kifo kinachoshukiwa ni cha kujiua mwwenyewe. Alikuwa na umri wa miaka 63.
 Kwa mujibu wa polisi wa Marin huko Calofornia, Marehemu Williams alikutwa hana fahamu huku akiwa hapumui majira ya saa sita za mchana Jumatatu nyumbani kwake Tiburon, kufuatia simu ya dharura iliyopigwa polisi hapo. Alitangazwa amefariki dunia saa sita na dakika mbili baada ya wahudumu wa huduma za dharura kufika. Alionekana hai kwa mara ya mwisho Jumapili.
 Uchunguzi wa kifo chake unaendelea, lakini ofisi ya Sheriff  inashuku ni kifo cha kujiua mwenyewe kwa dawa ya asphyxia. Msemaji wa familia Mara Buxbaum amesema kwamba Williams alikuwa na tatizo lam usongo wa mawazo (depression) hivi karibuni. Ametoa ujumbe wa familia kwamba wangependa wasibugudhiwe katika wakati huu mgumu wa msiba
 Mke wa marehemu Susan Shneider amekaririwa akisema kwamba: “Asubuhi hii nimempoteza mume, rafiki yangu mkubwa wakati dunia imempoteza msanii wake kipenzi. Nimevunjika moyo kabisa. Kwa niaba ya familia ya Robin, tunaomba kusiwe na bugudha wakati huu mgumu. Tunatumai shabaha ya wote haitolenga katika kifo cha Robin bali katika muda wake wa furaha na vicheko alivyotoa kwa mamilioni ya watu”
  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Jamani. Mungu amjalie Robin Amani. So sad. Mungu aitie nguvu familia yake.

    ReplyDelete
  2. Very sad.
    He made us laugh, but inwardly he was a sad man troubled by depression.He once said that God gave man a p---s and a brain but unfortunately not enough blood supply to run both at the same time.To me every time a saw a macho or a proud man, I remembered that
    Inna Lilah wainna.......

    ReplyDelete
  3. It is sad news, he was funny and loving person, I watched his movies. He will be missed by so many people. God please rest his good soul.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...