Na John Gagarini, Kibaha

BAADA ya dereva wa Texi Richard Ponera (36) mkazi wa Mwendapole wilayani Kibaha mkoani Pwani kupotea kwa siku nane amepatikana akiwa ameuwawa na kuporwa gari alilokuwa akiliendesha.

Marehemu ambaye alikuwa akifanyia shughuli zake kwenye kituo kikuu cha Mabasi cha Maili Moja wilayani humo alipotea Agosti 6 Mwaka huu majira ya saa 1 usiku alipokodishwa na watu wawili wasio fahamika waliojifanya kuwa ni wateja.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani humo Mrakibu Msaidizi wa Polisi (SSP) Athuman Mwambalaswa alisema kuwa mwili wake ulitupwa vichakani.

Kamanda Mwambalaswa alisema kuwa mwili wa marehemu ulikutwa huko eneo la Mihande Mashambani Mlandizi wilayani Kibaha ukiwa umeharibika vibaya huku gari alilokuwa akiendesha lenye namba za usajili T 905 BHT aina ya Corolla nyeupe.
“Chanzo cha mauaji hayo ni katika kuwania mali ambayo ni gari hilo ambalo halijapatikana na hakuna mtu ambaye amekamatwa hadi sasa na bado uchunguzi unaendelea kuwatafuta watu waliohusika na tukio hilo,” alisema Mwambalaswa.
Alisema kuwa jeshi hilo linaendelea kufuatilia juu ya tukio hilo na halitasita kumchukulia hatua kali za kisheria watu waliohusika na tukio hilo la kusikitisha, marehemu alizikwa juzi na ameacha watoto wawili ambao ni Ruben (14) anayesoma kidato cha kwanza St Anne na Kontrada anayesoma darasa la sita shule ya Msingi Jitegemee Jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. R.I.P roho inauma sana...masikini kwanini wamemuua??si wangechukua tu wakamuacha jamani....Nadhani kuna haja ya kubadiri mfumo wa Takci...ikiwezekana ziunganuisha...[Centralized] ambapo mkodishaji lazima aache contacts zake sio kwa dereva....hii itasaidia....Ngoja turudi tuje kuokoa maisha ....watu wanaangamia bila hatia....hawa watu wakikamatwa ni kuwang'oa ndimi zao kwa koleo tu....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...