DIWANI wa Viti Maalum Msasani jijini Dar es salaam, Mhe. Kuluthum Sagamiko ameandaa warsha kwa
ajili ya wenyeviti na makatibu wa Umoja wa Wanawake (UWT) wilaya ya
Kinondoni kwa ajili ya mafunzo ya kujiimarisha kichama na ujasiriamali
kwa wanawake.
Warsha hiyo ilifanyika Dar es salaam jana, ambapo jumla ya viongozi
hao kutoka kwenye kata 34 za wilaya hiyo walishiriki na kuweka
mikakati ya pamoja.
Akifungua warsha hiyo, Naibu Katibu Mkuu Bara Umoja wa Wanawake
Tanzania (UWT), Eva Mwingizi, aliwataka kuwa mstari wa mbele na
kusimama katika nyanja zote ikiwemo siasa na biashara bila woga.
Alisema uwiano sawa wa asilimia 50 kwa 50 katika uongozi hauwezi
kufikiwa endapo wanawake wenyewe watasita kujitokeza kugombea nafasi
mbalimbali.
"Nimefurahi leo kuwaona wanawake wamekutana pamoja, kwa sababu warsha
kama hizi zinawajengea uwezo,kina mama wanaweza na wakijengewauwezo
basi wanafanya vizuri katika nyanja zote.
"Kina mama ni mtaji mkubwa popote pale, ni tegemeo kwenye maeneo
mengi, hawa ni jeshi,ukitaka kufanikisha jambo, na kuwatumia kinamama
basi jambo hilo lazima lifanikiwe, kwahiyomafunzo ya kufanya
wajitambuezaidi ni muhimukwao,"aliongeza.
Alisema ingawa UWT ipo kisiasalakini walifikiria kuwainua kina mama
kwa kuanzisha kitengo cha miradi, ambapopamoja namambomengine
kinawaunganisha na taasisi mbalimbali za mikopo ilikuinua biashara
zao.
Naye muandaaji wa warsha hiyo, Diwani wa Viti Maalum Msasani, Kuluthum
Sagamiko,alisema lengo ni kuwajengea uwezo wanawake hao wanaotoka
katika kata, kwakuwandiowenye watu .
"Pia wajitambue nakujipanga nachangamoto hususan cha uchaguzi na
maisha kwa ujumla, hasa wakati huukuelekea katikachaguzi za
kitaifa,"aliongeza.
Licha ya kupata mafunzo ya kisiasa,Kuluthum alisema pia kunamkufunzi
wa mamboya biashara, ili kuleta msukumozaidi,kwa kuamini kuwa mwanamke
mwenye uchumi ananguvu zaidi.
"Kwenye wilaya yetuyaKinondoni, tumepoteza majimbo mawili na kata 11,
kupitia wanawake hawa, wenye nguvu nauelewa itakuwa rahisi kurudisha
maeneo tuliyopoteza kwa upinzani,"alisema.
Makatibu wa UWT wakisikiliza watoa mada (hawapo pichani) wakati wa warsha hiyo
Diwani wa Viti Maalum Msasani jijini Dar es salaam, Mhe. Kuluthum Sagamiko (wa pili kushoto) akiwa na viongozi wenzie meza kuu. Wa pili kulia ni Mgeni rasmi, Naibu Katibu Mkuu Bara Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Mama Eva Mwingizi.
Hongera Mama Diwani pigania maendeleo ya akina mama zetu!!
ReplyDelete