Mtangazaji mahiri wa habari za michezo wa siku nyingi Maulidi Baraka
Kitenge amejiunga na kituo cha radio kiitwacho EFM 93.7
kilichopo Kawe jijini Dar Es salaam leo.
Kutokana na tafiti ya ipsos ya mwaka 2013,inasemekana kuwa
mtangazaji huyo wa zamani wa kituo cha redio one,ndie
mtangazaji bora wa michezo nchini Tanzania.
Mkurugenzi wa vipindi wa Radio EFM,Dickson Ponela,ameeleza
kufurahishwa kwake kwa mtangazaji huyo kinara kuhamia katika
kituo hicho.
“Mpaka sasa Maulidi Kitenge ameshasign mkataba na kituo chetu
na anatarajia kusikika hivi karibuni katika kipindi cha michezo
hapa EFM”, alisema mkuregenzi huyo.
Maulidi Kitenge au jezi nambari tisa mgongoni, amejiunga na
magwiji walio bobea katika fani hiyo akiwemo Dizo one,Dennis
Sebo,Sos B,Kanky Mwaigomole na Dj Majay.
Mtangazaji mahiri wa habari za michezo,Maulidi Baraka Kitenge akisaini Mkataba wa kazi na kituo cha radio kiitwacho EFM 93.7 kilichopo Kawe jijini Dar Es salaam.Kushoto ni Mkurugenzi wa vipindi wa Radio EFM,Dickson Ponela.
Mtangazaji mahiri wa habari za michezo,Maulidi Baraka Kitenge akipeana mikono na Mkurugenzi wa vipindi wa Radio EFM,Dickson Ponela wakati wa kubadilishana mikataba baada ya kusainishana jioni hii katika makao makuu ya Radio hiyo,yaliopo Kawe jijini Dar es Salaam.
hongera sana mzee wa bila kupepesa macho aka namba tisa mgongoni...mau wa kitenge. kizuri unachokipata sio utakachokuja kupata....maisha changamoto na sio kuwa maarufu tu.....kazi njema na mungu akuongoze
ReplyDeleteMaulidi wakati wako huu wakuvuna ulichokipanda umefata pesa hukutaka umaaurufu wa radio
ReplyDeleteHiyo ndo maanake, ukiwapunja mshahara wanahama.Because you are not the only.
ReplyDeleteKweli ukubwa wa pua, sio wingi wa . . . . . . . .
ReplyDeleteHongera mau... lakini hiyo radio sijawahi isikia... tutakumiss radio one
ReplyDeleteKila la kheri katika changamoto mpya,natumaini mashabiki wako watakufuata huko
ReplyDeletePesa sio mchezo,ata lampard anajua.Teh teh teh
ReplyDelete