Mtangazaji mahiri wa habari za michezo wa siku nyingi Maulidi Baraka Kitenge amejiunga na kituo cha radio kiitwacho EFM 93.7 kilichopo Kawe jijini Dar Es salaam leo.

Kutokana na tafiti ya ipsos ya mwaka 2013,inasemekana kuwa mtangazaji huyo wa zamani wa kituo cha redio one,ndie mtangazaji bora wa michezo nchini Tanzania.

Mkurugenzi wa vipindi wa Radio EFM,Dickson Ponela,ameeleza kufurahishwa kwake kwa mtangazaji huyo kinara kuhamia katika kituo hicho.

“Mpaka sasa Maulidi Kitenge ameshasign mkataba na kituo chetu na anatarajia kusikika hivi karibuni katika kipindi cha michezo hapa EFM”, alisema mkuregenzi huyo.

Maulidi Kitenge au jezi nambari tisa mgongoni, amejiunga na magwiji walio bobea katika fani hiyo akiwemo Dizo one,Dennis Sebo,Sos B,Kanky Mwaigomole na Dj Majay.
Mtangazaji mahiri wa habari za michezo,Maulidi Baraka Kitenge akisaini Mkataba wa kazi na kituo cha radio kiitwacho EFM 93.7 kilichopo Kawe jijini Dar Es salaam.Kushoto ni Mkurugenzi wa vipindi wa Radio EFM,Dickson Ponela.
Mtangazaji mahiri wa habari za michezo,Maulidi Baraka Kitenge akipeana mikono na Mkurugenzi wa vipindi wa Radio EFM,Dickson Ponela wakati wa kubadilishana mikataba baada ya kusainishana jioni hii katika makao makuu ya Radio hiyo,yaliopo Kawe jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. hongera sana mzee wa bila kupepesa macho aka namba tisa mgongoni...mau wa kitenge. kizuri unachokipata sio utakachokuja kupata....maisha changamoto na sio kuwa maarufu tu.....kazi njema na mungu akuongoze

    ReplyDelete
  2. Maulidi wakati wako huu wakuvuna ulichokipanda umefata pesa hukutaka umaaurufu wa radio

    ReplyDelete
  3. Hiyo ndo maanake, ukiwapunja mshahara wanahama.Because you are not the only.

    ReplyDelete
  4. Kweli ukubwa wa pua, sio wingi wa . . . . . . . .

    ReplyDelete
  5. Hongera mau... lakini hiyo radio sijawahi isikia... tutakumiss radio one

    ReplyDelete
  6. Kila la kheri katika changamoto mpya,natumaini mashabiki wako watakufuata huko

    ReplyDelete
  7. Pesa sio mchezo,ata lampard anajua.Teh teh teh

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...