Halmashauri zote nchini zinawajibika kutenga maeneo kwa ajili ya shughuli za maendeleo ya vijana
pamoja na kuwatengea vijana asilimia 5 ya mapato ya halmashauri husika kwa ajili ya kuwezesha
shughuli hizo.
Hayo yamesemwa jana ( leo) Mkoani Dodoma Wilaya ya Nchemba na Afisa Vijana wa Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo, Bi. Amina Sanga katika mafunzo ya Vijana wa Halmashauri ya Wilaya
hiyo kuhusu mikopo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana.
Bi. Amina alisema kuwa vijana ndiyo nguvu kazi ya taifa na kwa maana hiyo wanatakiwa waongozwe
na wawezeshwe ili kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo kwa lengo la kujikwamua katika
umaskini.
“Vijana wanatakiwa kuhamasishwa kuunda na kujiunga katika vikundi vya uzalishaji mali na kuunda
SACCOS za vijana ili waweze kupatiwa mikopo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana kwa ajili ya
kuongeza mitaji na kupanua uzalishaji”. Alisema Bi Amina.
Aidha aliwashauri kujituma na kuchangamkia fursa mbalimbali ikiwemo mikopo inayotolewa kupitia
Mfuko wa Maendeleo ya Vijana.
“Nchemba ni miongoni mwa Wilaya zenye fursa nyingi kwa vijana ikiwemo kilimo ambacho kimekuwa
kikitoa ajira kwa Watanzania zaidi ya asilimia 70 waishio vijijini”.Alisema Bi. Amina
Akiongea na vijana katika moja ya ziara ya ukaguzi wa miradi hiyo alisema vijana wanayo nafasi kubwa
ya kuleta maendeleo katika maeneo yao hivyo wanapaswa kuwa wabunifu wa miradi itakayowaingizia
kipato.
Pia aliwataka kuhakikisha kuwa wanasajili vikundi vyao ili viweze kutambulika kisheria na pia wajiunge
katika SACCOS ya vijana ili iwe rahisi kupatiwa mikopo ya kuendeleza shughuli zao za uzalishaji mali.
Katika mafunzo hayo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nchemba Bw. Boniface Mandi
amewashauri vijana waachane na matumizi ya madawa ya kulevya na kutumia fursa mbalimbali
zinazotolewa na serikali.
Kwa upande wa Vijana hao alishukuru Idara ya Maendeleo ya Vijana kupitia Wizara ya Habari,
Vijana,Utamaduni na Michezo kwa kuwapatia mafunzo hayo kwani wamekuwa wakikutana na
changamoto mbalimbali katika utendaji wao wa shughuli mbalimbali za ujenzi wa Taifa.
Afisa wa Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni na
Michezo Bi. Amina Sanga akitoa mada katika Mafunzo ya Vijana wa Halmashauri ya Wilaya ya Nchemba
mkoani Dodoma kuhusu Mikopo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana.
Picha na Benjamin Sawe
Halmashauri zikitekeleza haya vijana watapatiwa msaada na kuwezeshwa ili wawe sehemu ya uchuni wa halmashauri. Halmashauri pia zisajili vijana ili zijue zina vijana wenye taaluma gani katika sehemu zao, hii itasaidia kufungua pia fursa za vijana hawa wakiwa kwenye makundi katika kuleta bidhaa na huduma zinazotakiwa na halmashauri au kama kuna mainjinia kwa mfano kuhusishwa katika kazi za muda za ujenzi wa nyumba, ukandarasi wa barabara etc. Asilimia kubwa zaidi za kazi hizi zitengewe kwa ajili ya vijana kwenye halmashauri kufuatana na taaluma na uwezo wao.
ReplyDelete