Mwenyekiti wa ALAT Mkoa wa Dodoma Mhe: Athuman Mwenda akipata maelezo ya
kina jinsi ya uandaaji wa taarifa za hali ya hewa kwa wakulima ili kufanikisha kauli mbiu ya mwaka huu
yenye ujumbe wa ‘Matokeo Makubwa Sasa’-Kilimo ni Biashara, vilevile Mamlaka inatekeleza mkakati
wa Taifa wa KILIMO KWANZA.Maelezo hayo yalikuwa yakitolewa na kwa Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti
na Matumizi Dkt. Ladislaus Chang’a katika banda la Mamlaka ya Hali ya Hewa kwenye maonesho ya
NaneNane 2014, viwanja vya Nzuguni-Dodoma.
Mwenyekiti wa ALAT Mkoa wa Dodoma Mhe: Athuman Mwenda akipata maelezo
mafupi ya uangazi wa hali ya hewa ardhini kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti na Matumizi Dkt.
Ladislaus Chang’a alipotembelea banda la Mamlaka ya Hali ya Hewa, katika maonesho ya NaneNane
2014, viwanja vya Nzuguni-Dodoma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...