Majaji Bw. Venance Bahati (kushoto) na Bi. Costansia Gabusa (kulia) wakijadiliana
jambo wakati wa kufanya tathmini ya mradi wa ukingo uliojengwa pembezoni mwa
bahari kwa ajili ya kuzuia mmomonyoko katika eneo la Mwarongo jijini Tanga.
Ukingo huo umejengwa kwa msaada wa kampuni ya utafutaji wa mafuta na gesi ya
Afren PLC.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Tongoni Bw. Mzihili Abeid (kushoto)
akitoa maelezo mbele ya majaji waliotembelea maabara ya shule hiyo. Maabara hiyo
imejengwa na kampuni ya utafutaji wa mafuta na gesi ya Afren PLC.
Msimamizi wa kampuni ya utafutaji wa mafuta na gesi ya Afren PLC Bw. Ahmed
Omar (kulia) akizungumza na jopo la majaji na sektretarieti kwenye maabara ya
shule ya sekondari ya Tongoni iliyofadhiliwa na kampuni hiyo.
Jaji Venance Bahati (katikati) akiteta jambo na msimamizi wa kampuni ya utafutaji
wa mafuta na gesi ya Afren PLC Bw. Ahmed Omar (kulia). Kushoto ni Jaji Costansia
Gabusa.
Msimamizi wa kampuni ya utafutaji wa mafuta na gesi ya Afren PLC Bw. Ahmed
Omar (kushoto) akizungumza na majaji walipotembelea maabara ya Shule ya
Sekondari ya Mabokweni jijini Tanga ambapo kwa sasa kampuni hiyo imejitolea
kuwajengea maabara ya kisasa.
Mkurugenzi wa kampuni ya Dawson Food Products Ltd iliyopo wilayani Mkinga
mkoani Tanga Bw. Burhani Taibali (kulia) akizungumza na majaji pamoja na
sekretarieti iliyotembelea kampuni hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...