Mkurugenzi Mkuu wa Drive Dentsu, Mr Cheriff Tabet (kushoto)akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa ofisi yao Dar es Salaam. Kulia kwake ni Meneja Uendelezaji wa Biashara na Masoko Mapya, Rami El Khalil.

Mkurugenzi Mkuu wa Drive Dentsu, Mr Cheriff Tabet (katikati)akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa ofisi yao Dar es Salaam. Kulia kwake ni Meneja Uendelezaji wa Biashara na Masoko Mapya, Rami El Khalil, na kushoto ni Meneja Mkuu wa Drive Dentsu Tanzania, Terry Greenwood.


========  ========  ========= 
             
Dar es Salaam, 26-August, 2014: Kampuni ya Drive Dentsu, imefungua ofisi zake mpya jijini Dar es Salaam katika jitihada za kusogeza huduma zake kwa wateja wake katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Ikiwa ni kampuni iliyotanda nchi zaidi ya 110, Drive Dentsu ni sehemu ya muunganiko wa kimataifa wenye zaidi ya wafanyakazi 37000 na ofisi 160 duniani kote, muunganiko ambao unaleta pamoja ujuzi, maarifa na vitendea kazi vyenye kuhakikisha inawapa wateja wake huduma zenye ubora wa hali ya juu.

Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Bw. Cheriff Tabet, Mkurugenzi Mkuu wa Drive Dentsu, amesema ufunguzi wa ofisi mpya ya Drive Dentsu jijini Dar unalenga kutoa suluhisho la ubunifu kwa makampuni na bidhaa za kitanzania.

Bw. Tabet amesema pamoja na kuwekeza nchini Tanzania, Drive Dentsu imelenga kujipanua katika masoko mengine katika ukanda huu ili kuhakikisha wanakidhi mahitaji yao kwa kutoa suluhu kwa changamoto zote za kibiashara.

 “Katika ukanda wa Afrika Mashariki, uchumi wa Tanzania umekua ukikua kwa kasi kubwa pamoja na ongezeko la uzalishaji wa bidhaa nyingi jambo ambalo linakuza mazingira yenye ushindani hivyo kufanya kuwepo na uhitaji mkubwa wa ubunifu katika kuwafikia wateja’  anasema Bwana Tabet.

Tabet pia anasema kuwa Drive Dentsu inaleta uzoefu wake mkubwa, nchini Tanzania, ambao umewawezesha kutwaa tuzo 17  za kimataifa na kitaifa katika tasnia ya ubunifu wa matangazo. Naye Bw. Rami El Khalil, Meneja Mkuu wa Masoko na Maendeleo ya Biashara wa Drive Dentsu anasema Tanzania ni nchi yenye fursa nyingi kutokana na uchumi wake kuwa imara hivyo ni sehemu nzuri kuwekeza.

‘Drive Dentsu itaweka muhimili mpya katika tasnia hii ikiwa na mtazamo mpya wenye kusaidia chapa kujidhihirisha na kutambulika kwa watumiaji wake’ anasema Bw. Rami. Pia Drive Dentsu wamewekeza katika wataalam mahiri walioko nchini, hili linajidhirisha walipomteua Terry Greenwood kuwa Meneja Mkuu wa kampuni hiyo nchini Tanzania.

Terry mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 41 katika tasnia ya mawasiliano, amepata uzoefu huo katika makampuni mbalimbali huko Amerika, China na Mashariki ya Kati. Pia kwa miaka saba sasa amekuwa akifanya kazi na Drive Dentsu.

Kwa uzoefu wake na ushirikiano kutoka kwa mtandao wa Drive Dentsu kimataifa tunaamini ataleta mapinduzi katika tasnia ya utengenezaji matangazo. Wateja wa Drive Dentsu kwa sasa ni kama Zantel, Moov, Moneygram, Radisson Royal Hotel, Daihatsu, Hitachi, Jammal Trust Bank, Toshiba, Lexus, Bridgestone, Jumeirah dot Shabaka, Toyota, Virgin, Abdul Latif Jameel na Vitaene C.

‘Ofisi zetu nchini Tanzania zitakuwa ni sehemu ya kuimarisha muunganiko wetu kimataifa, pia itaiwezesha Drive Dentsu kuwasaidia wateja wetu kukabiliana na mabadiliko ya kila siku katika biashara’ anamaliza Bwana Rami. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Hii yanikumbusha atikali nyingi zinavyoonyesha ufundishaji wa uhadishi wa habari Bongo bado tuko mbali.
    Sasa mtu utaandika ahabari kuhusu kampuni bila kusema biashara gani wanajishughulisha nazo? umetaja wakuu wao, ukasema wana wafankyazi kadhaa, ukasema idaidi ya nchi waliko na ofisi, uka nakiri matamshi bioa kusema la msingi????
    mara kwa mara utaoan wahandisha wanatuwekea picha za viongozi na habari chini ya picha " fulani akimwambia jambo???"
    kazi ipo ndugu..wapigananaji kweli inatakiwa kukazi uzi..uhandishi wa habari kupasha na keulemisha..sasa Drive Dentsu ni mdudu gani..ndio tumeona meeneja na dk..

    ReplyDelete
  2. Drive Dentsu ni kampuni inashughulika na nini?

    ReplyDelete
  3. Naoana itabidi ku google.hi.kampuni maana kiukweli habari haikukamilika....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...