Naomba kutoa pendekezo kwa Wizara husika,Wakuu wa mikoa ,Wakuu wa wilaya , Mameya na Halimashauri husika juu ya uchafu unaozidi kukidhili kila siku kwa baadhi ya maeneo ya miji mikuu na karibu na mahoteli yanayolisha wasafiri kuelekea mikoani, nadhani na wao pia watakuwa mashaidi juu ya mifuko ya plastic inayozagaa ovyo barabarani, na mitaro ya maji iliyojaa mifuko na maji machafu, na mchanga iliyoachwa baada ya kuziburiwa katika mitaro,
Ombi langu kwa
Serikali itoe ajira kwa vijana wasio na kazi kuokota uchafu kila siku hata kwa masaa mawili kila siku kwa kuwalipa pesa kidogo na pia wawape jukumu la kuwakamata wahusika wanaotupa uchafu hovyo ili walipishwe faini, na kila kijana atakaye kamata mtu akitupa uchafu pesa atakayomtoza iwe yake ya mfukoni kuwapa motisha kujitolea kuwadhibiti wanaotupa hovyo uchafu, na kwa upande wa mabasi waweke ndoo ya kukusanyia uchafu kwenye mabasi yote hata kama ni daladala, na waandike matangazo ya kutotupa uchau nje ya gari au basi. mimi nahisi kila mtu akiwa anadhamana ya kumkamata mtu na kumlipisha faini itasaidia sana maana kila mtu atakuwa akimuogopa mwengine,
na kwa wazizi au walezi tuwafundishe watoto wetu tokea wadogo kutotupa uchafu ovyo,
Huu ndiyo mtazamo wangu natumaini wengi watakuwa na mtazamo tofauti na maoni yao tofauti, karibuni kwa kuchangia
Mdau anaekerwa na Uchafuzi wa Mazingira.
Uchafu umezidi shauri ya uzembe...ila wakuu wako kwenye ufisadi
ReplyDeleteUsafi ni tabia. Inaonekana tabia yetu ni watu wachafu tu!
ReplyDeleteIsingetakiwa kubembelezana kwenye hili.
Wazo lako ni zuri, ila kwa serikali ipi?? Maana mara kadhaa tumeona jinsi ambavyo serikali imeshindwa kusimamia sheria ambazo zipo kuhusu hili. Mifuko ya plastiki ilizungumzwa na viongozi wakuu wa serikali lakini hamna kilichofanyika! Jirani yetu Kaskazini/Magharibi wamewezaje?? ...ukali kuanzia juu!
Jiji lenyewe ambalo ndio kioo cha taifa mifereji ya maji machafu inamwaga maji tena katikati ya barabara, huku viongozi (maMeya na wengine) wakifanya usafi wa maigizo wa kupigwa picha za mnato na za video!
Wanasema samaki huoza kuanzia kichwani, kama maMeya na wenzenu msipoonekana kivitendo kukerwa na hili, labda mpaka......
The mdudu,tupo pamoja mdau ila mm nauliza hivi nahao viongozi wanaolipwa mipesa wako wapi? Kuanzia mkuu wa kitongoji hadi mkuu wa mkoa au ndio hawajui walifanyalo? Wao kula pesa tu za walipa kodi....hasa hasa mkoa wa DAR ni aibu kubwa huu mkoa kusikia eti una MKUU WA MKOA,MEYA,WABUNGE,MADIWANI,na pia wakazi wote wa mkoa wa dar wote ni wachafu coz haiwezekani wote kulizika katika hari ya UCHAFU ULIOKISILI kama hivyo huku wakazi wote wa jiji hilo mkiwa mmelizika kabisa,ni bora tutukanane sasa ndio labda watu watastuka nakuzinduka usingizini,nchi zingine za wezetu nchi kuwa katika hali ya UCHAFU NI KOSA LA JINAI sasa kwanini Tanzania ni CHAFU NCHI NZIMA? Tuamkeni natuseme sasa Tanzania yetu Uchafu BASI
ReplyDeleteDa! hizi takataka kweli zinakera jamani. Yaani kama mdau wa pili alivyosema, kweli viongozi husika tunashindwa kuwaajili vijana wanalanda landa mitaani ambapo wangefanya kazi hii ya kuzoa taka taka kila mahali wakalipwa ujira wao? walau hata kwa saa iwe tu 1000 kama kuna ushindikani wa pesa. Kweli tunaleta aibu Tanzania. Uchafu imekuwa ndo sehemu yetu ya maisha kweli inasikitisha na ujambazi hautaisha sababu vijana wengi hawana ajira na kumbe wangeajiliwa kwa hata kazi za kuzoa taka. Mkae mtafakari wahusika wa idara hiyo.
ReplyDeleteTusipote nguvu bureee kupiga kelele za kutaka kukomesha uchafu: Tumeridhika na hali hii na tutakapochoka yenyewe itaondoka.
ReplyDelete