Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Sasa, kama huyo jamaa hakutaka kuwa kwenye video, si angekaa pembeni tu? Nadhani ni dharau kama unajaribu kuhamasisha kitu halafu unaonesha kutokuwa na interest.

    ReplyDelete
  2. Tafadhali taarifa kama hizi zitolewe mapema ili tuweze kujipanga, sasa next week ni karibu mno. Lakin napenda kuwapongeza kwa hatua hii muhimu sana.
    Mungu ibariki Tanzania

    ReplyDelete
  3. Kwanza, Mheshimiwa Rais kashasema kazi za watu wa diaspora ni kuingia kwenye blog kupoteza muda na kutofanya cha msingi. Kwa kifupi, ametusi jamii nzima ya diaspora kwa kutumia takwimu ndogo ya wafanyao hayo. Je amefanya uchambuzi yakinifu kujua kama hao wachafua hewa ni watu wa diaspora?

    Pili, Ninapenda kujua hiki kikao cha wana diaspora kinachoitishwa kwa juma lijalo kimeandaliwa kwa muda gani? Kuna uwakilishi wa kweli ulioandaliwa? au ni uuzaji wa sura na kwenda kupewa dondoo za WESTADI?

    Turudi kwa Mheshimiwa Rais, chonde chonde jifunze kwa Rais Uhuru, yeye aliongea na wana diaspora wa Marekani, wewe ulihutubia wana diaspora.

    Cha msingi Mtukufu Rais jaribu kuunganisha Watanzania wawe wamoja, walio nyumbani na nje ya nchi; nia yetu ni moja nchi yenye maendeleo, Uhuru na Haki Sawa kwa kila Mtanzania.

    Mdau NY.

    ReplyDelete
  4. Juzi nimemsikia mhemishimiwa Raisi akisema kuwa uraia pacha wana-diaspora hawako serious. Sasa mnaisitiza na kuwaita wanadiaspora na kuona umuhimu wao na kuwa wana mchango kwenye Taifa. Kwanza Taifa linapata mapato mengi kutoka kwa Watanznia amabo wako nje. Sasa wanadiapora bila uraia pacha ni vipi?? Mbona siielewi hii serikali ya Jamhuri pamoja na Raisi, mnadhani Kenya na Uganda wansonga mbele kwa sababu gani??Hivi hii kasumba ya chuki Wa-Tanzania itaishia lini??.Mwanadiaspora na mwanaataaluma-Sweden.

    ReplyDelete
  5. Hapo ajenda kuu mie nshaijua tayari bila hata kutafuta meno......ngoma pacha tu hakuna kingine...au mengine kama kufunika funika.......

    ReplyDelete
  6. hivi watanzania bado tunafikiri kwamba mwekezaji ndio ataleta maendeleo.hawa diaspora ndio resources kubwa tuliyonayo.Tanzania kila mtu anafikiri sawa tu.Hakuna kufikiri wala kujituma.Hii ni zamu ya watanzani walio njee kupewa fursa.Namshkuru Kikwete kwa kuona hili.This is a big favor to our country.

    ReplyDelete
  7. Mbona matangazo ya mkutano yalikuwa hapo juu siku nyingi tu. Hakuna haja ya watanzania walioko nje kutaka kuhakikishiwa kama wao ni wadau wa nchi hii au la. Ukijua asili ya uraia wako ilikuwa huku ni upendo wa nchi yako utakaokusukuma kuchangia maendeleo au kujiendeleza wewe mwenyewe na jamii yako ukitumia fursa zinazopatikana nchini.

    ReplyDelete
  8. Wazo zuri lakini mmetoa muda mfupi sana kwa wanadiaspora kujiianda .Si rahisi kwa mtu kupanga safari kwenye kipindi cha wiki moja....Next time please toeni tangazo miezi kadha kabla...Mdau ughaibuni

    ReplyDelete
  9. Jambo la ajabu Wana diaspora wa Kitanzania ni Tofauti na wa nchi zingine huko Majuu!

    Diaspora wa Ki-TZni watu wenye majivuno, much know sana, Dharau nyingi na watu wa kujikweza sana mfano halisi ni kauli za 'kunya' zinazotolewa na hao Wadau Wawili hapo juu No. 3 Mdau wa NEW YORK na No.4 Mwanataaluma Mdau wa Sweden.

    Hivi kweli ninyi adabu za Kitanzania mngali nazo?, mnaweza kutoa matamshi kama hayo kwa Kiongozi wenu hasa Raisi wa nchi?

    KWA KUWA RAISI JAKAYA KIKWETE NI KIONGOZI MAKINI SANA,,,(PIA MKUMBUKE JK HANA UTAMADUNI WA KUMHCELEWESHA MTU, YEYE NI MUWAZI NA MKWELI KUPITA KIASI),,,AMESHA WASOMA MUDA MWINGI SANA NA HUO MTAZAMO WAKE JUU YA SUALA LENU LA DIASPORA LA URAIA PACHA AMESEMA HAMPO SERIOUS !!!

    MSIFANANISHE RAISI UHURU KENYATTA WA KENYA NA RAISI JAKAYA KIKWETE WA JAMHURI MYA MUUNGANO WA TANZANIA,,,ANGALIENI KWANZA KTK MKUTANO WA MAREKANI US-AFRICA LEADERS FORUM JK ALIKUWA HIGH TABLE A.K.A MEZA KUU MBELE WAKATI RAISI UHURU KENYATTA ALIKUWA KWENYE WAJUMBE WA KAWAIDA WA MKUTANO,,,HIVYO WEWE MDAU WA NEW YORK ACHA DHARAU ZAKO KABISA DHIDI YA RAISI JK HAPA WATU WA TEAM KIKWETE NA TEAM TANZANIA TUPO HUMU JAMVINI!

    HATA MKICHUKIA KWA KAULI HIYO HUO NDIO UKWELI WENYEWE!

    ReplyDelete
  10. Mdau uliyechanganya herufi kubwa na ndogo hapo juu huku ukiwasema wengine wakati na wewe umerudia humohumo ku-generelise kuwa woote wana_Diaspora wako hivyo kama hao wa NY na Sweden, naomba ukane kauli yako! La sivyo hapa hatufiki!

    Jengeni hoja na sio kuongea sababu za rojorojo maana hapa unataka kutukumbusha mambo ya enzi za utumwa kati ya "field negro" na "house negro".

    Njooni msikilize hoja zilizoko huku Dar, watakaohudhuria waone ni mchango gani wanaweza kutoa katika kujinufaisha kiuchumi na hivyo kukuza uchumi wa taifa!

    Nyumbani ni nyumbani, kuna utamu wa kuwekeza kwako. Hatari ya kubaki kwenye hoja dhaifu ndo yale yale tunashindwa hata kuelewana kwenye maswala ya kitaifa (Katiba).

    Njooni kwa mtakaopata nafasi, ila tutumie busara kwenye ku-address kasoro zinazoweza kujitokeza. Tukikwazana tutachekwa wote kama wa-TZ, hutaweza kujibadili uraia.

    Hakika, kwa wana-Diaspora mkiweka akili zenu kwenye changamoto za hapa TZ, nina uhakika mbele ya safari tutajivunia kuwa wanetu wa ng'ambo walitutoa!!

    ReplyDelete
  11. Mdau no 9 nimekukubali.
    Dharau na majivuno haisaidi katika mjadala wowote. JK hawezi pekee kutetea mjadala wa wana diaspora ila weneye inabidi tufanye hivyo, ndicho alichotuasa. Zaidi tujue kuwa uraia pacha unategemea mapendekezo ya sheria ya uraia kubadilishwa baada ya mswaada..sio haki ya mtut yeyote..sasa lawama zitoke wapi kwa JK kama amesema ukweli..toka hoja za uraia pacha ili kuwepo na msingi wa kubadili sheria.
    Malumbano yoyote yakishaleta dharau na majivuno, uvunjika, na hapa ikivunjika wa kuumia nani? sio mtania aliye na uraia wake wa Kibongo, na wana diaspora tunataka kuwili..uraia pacha..sasa kongamana kama hilo tuombe litoe changa moto ya kuendeleza mazunumzo na kuto chachu inayotakiwa kuwa hoja y auraia pacha inafaa kuendelezwa..na hapo nidhamu na ustaarabu vinahitajika.
    bravo mdau hapo juu ( na 9)

    ReplyDelete
  12. The mdudu,mm huwa naona mbali sn kama hayati mpendwa wetu K Nyerere,kwanza ngoja niwachambue waliokua kule USA au kwa Obama na hapa nilipo mm The mdudu UK au kwa mama wa kambo..Madada zetu wengi wao wanaishi na mamluki kutoka Lagos,Ghana,D R C,leo hii hao hao wanataka u.pacha mm naona mwende huko huko mlikoona kunafaa na muombe huo U.pacha na mkakumbane na Ebola kwakula nyani,panya,kenge na midudu mingine,ila siwalaumu sn coz dada zangu wengi hawapatani na shule sijui huko kwingineko lakini hapa Uk wengi walijisahau na maisha ya Benefit mpaka ilifika wakati walikua wanawafukuza waume zao ndani kwa jeuri ya pesa,lakini sasa hivi hapa hapakaliki coz hii serikali mpya imekata benefit zote so wadada zetu njaa mtu wanahaha,so tuwe makini na haya maswala ya Upacha wadada zetu kwaujinga wao wanataka kutuletea hao mamluki niliosema hapo juu ili wapate hizo passiport za TZ kisha wafanye ushenzi wao wa Madawa ya kulevya,na alichokisema Rais kikwete kule USA ni kweli kabisa huku wengi wao ni umbea kwenda mbele si wanaume wala wanawake wote same mm naiomba serikali uwaludishe watu wenye umuhimu kwa Taifa na wala sivinginevyo IFANYE USAILI MWENYE UJUZI ndio afaidike na Upacha na kama huna ujuzi wowote utakuwa mzigo kwa Taifa hakiyamungu hapa wengi wangeumbuka si wakaka wala wadada.mamluki wengine wakua nao makini ni WADOSI hawa ndio wataiangamiza NCHI msipokua makini,ni hayo tu kwa leo

    ReplyDelete
  13. Mdau hapo juu acha kutoa sababu pumba. siyo watanzania wote wanaoishi nje wanategemea mabwana wa ki-Nigeria, Ghana, wengi wao wanafanya kazi na kulipa kodi na pia tunalipa kodi tukituma pesa huko nchini lakini hamsemi kitu. Mbona wa-Tanzania wengi wanafanya biashara ya madwa ya kulevya na wako jela na hawana uraia pacha? Hizo rasilimali za Taifa zilizo ibiwa za EPA hao watu walikuwa na uraia pacha?? kwanini htukula changamato na kubadilka na kusonga mbele.Raisi Kikwete nampenda ila hotuba yake aliyoitoa Marekani ILINICHEFUA pale aliposema kuwa watu wa liko nje hatusemi na watu hawaoni umuhimu Wake?? Mbona War. Membe alipokuwa anahijiwa na mwandishi wa BBC au CNN hakusema hiyo sababu alisema wanaifanyia kazi kwenye Katiba mpya, kwanza alikuwa hana reason muhimu kwani aliwekwa kwenye kona. Michuzi ulibana comment yangu nilituma kwenye hotuba ya Raisi, Kwakweli watanzania tuna mawazo mgando, wenzetu wa Kenya wanapenda changamoto na pia wanapenda maendeleo.Hotuba ya Raisi Kenyatta ilikuwa inaongeala maendeleo kwa Wakenye na jinsi ya kuindeleza Kenya. Ndiyo maaana Tanzania watu hawafanyi kazi wanasubiria rsuhwa na meendeleoe hakuna hata kwa vutu visivyotaka rushwa watu wamekaa maofisini wanasubiri RUSHWA badala ya kufanya kazi.Mnadhani watu wasiofikiri si wanataka hela z achapu chapu ndio maana ma-unga yanawaharibu vijana na wanakamatwa kila leo , serikali inaficha takwimu zingine.
    Mdau na mwanataaluma Sweden

    ReplyDelete
  14. Nikitaka kucheka nasoma comment za post za Diaspora hapa sasa hata mada kwishakuwa diluted. Nilijua watu wa diaspora wajanja kumbe bora wale wa kijijini mtwara. Teh teh badilikeni watanzania acheni kuwekana uchi upenuni

    ReplyDelete
  15. Mdau no.8 ambaye umeandika kwa herufi kubwa. Kuwa Raisi si kama anafanyakazi zote kama Malaika wa Mbinguni na yeye ni binadamu kama mtu kakosea na kasema lugha ambayo hairidhishi akiambiwa ukweli asikasirike-HIZO NDIO CHANGAMOTO ZA UONGOZI. Kama mtu makini kwakweli Tanzania inatia aibu sasa hivi ukisafiri nje ya nchi na hizi kesi za madawa ya kulevya wanadhani wote ni wauza unga umakini wa Raisi ni pia kuafatilia na kukemea maovu na KUWASHUGHULIKIA ANAYO MAMLAKA. Kwa sasa Tanzania tunatia aibu ulimwengu mzima. Kukaa high table siyo hoja na hata kama ni Raisi makini. UHURI wa kuongea anao kila mtu. Mimi wa upande wangu nimeona ameongea lugha si nzuri au maelezo yake kuhusĂș Diaspora na URAIA PACHA SIKUYAPENDA. Kama ni hivyo wakati Mheshimiwa Membe akihojiwa na mtangazaji wa BBC au CNN ukiweza tafuta clip kwa MICHUZI uisikilze kwa nini uraia pacha Tanzania unachukua muda alijibu wanasubiri Katiba mpya angejibu watanzania hawako serious na aliwekwa kwenye angle na sababu alizokuwa anatoa zilikuwa hazina nguvu na alikuwa kama anabababaika sana. Raisi anaposema Watanzania hawako serious kazi yetu kuingia kwenye mablogu na kutukanana labda hayo mablogu ya UDAKU ambayo wengine hatuna muda wa kuyasoma. Ila kwa upande wangu ninaona wawakilishi waliowatuma kwenye Bunge natunavyoandika inatosha na pia kura tulizopiga wana diaspora wote ni nyingi napia kama wewe uko ndani utakuwa umepiga . Kwanza ni watanzania wangapi huwa wanapitia mablogu kuangalia comment wengi wanao-comment ni wana diaspora wa huku hao wanocomment upuuzi ni watu walioko huko Tanzania na pia watu wana roho zao wanazozijua wenyewe. Watu wanatoa sababu kuwa mali za Taifa zitaibiwa, mabilioni ya EPA yaliibiwa na wana-diaspora?? hela zilizoko kwenye account za uswisi ni za wana diaspora??kuna mengi yanayoendelea hayajafanywa na wanadiaspora ila likifika la URAIA PACHA ni kwamba MALI ZA TAIFA ZITAIBIWA, Mimi naona wezi wako huko2 kwanza wangewashughulikia na si kuwachekea na kuwaaachia- Raisi ni makini kwa shughuli zake, Mkubwa hakosei_ILA ANAAMBIWA UKWELI NA AKUBALI CHANGAMOTO huo ndo uongozi. TUJIFUNZE KUBADILIKA NA KUTOA MAWAZO MGANDO. Kwanza mimi nasema kama Tanzania tungekuwa tnafanya kazi kama wenzetu tungekuwa mbali sana. Ila sisi Wa-Tanzania tu WAVIVU NA KUPENDA RUSHWA. Nimefanya kazi serikalini Tanzania muda mrefu na huku pia nafanya kazi serikalini kuna tofauti kubwa sana na kazi proffesional na siyo kubeba maboksi-MUNGU IBARIKI TANZANIA,MUNGU IBARIKI AFRIKA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...