MABINGWA watetezi klabu ya mchezo wa Pool ya Top Land ya Mkoa
wa kimichezo wa Kinondoni jijini Dar es Salaam imemefanikiwa
kutetea Ubingwa wake katika fainali za mashindano ya mchezo huo
yajulikanayo kama “Safari National Pool Competition 2014” kwa
kuwafunga timu ya klabu ya Meeda 13-5, yaliyomalizika mwishoni
mwa wiki Mkoani humo na kuzawadiwa pesa taslimu Shilingi 800,000/
= pamoja na tiketi ya kuwakilisha Mkoa wa kimichezo wa Kinondoni
kwenye fainali za kitaifa zinazotarajiwa kufanyika Mkoani Kilimanjaro.
Nafasi ya pili ilichukuliwa na Meeda Pool Klabu na kuzawadiwa fedha
taslimu Shilingi 400,000/= na nafasi ya tatu ni Jaba Pool Klabu ambao
walijinyakulia fedha taslimu Shilingi 250,000/= na nafasi ya nne
ilichukuliwa na klabu ya JBS ambao walizawadiwa fedha taslimu Shilingi
100,000/=.
Upande wa mchezaji mmoja mmoja wanaume Salum Yusuf alifanikiwa
kutwaa ubingwa wa mkoa na kuzawadiwa fedha taslimu Shilingi
400,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha Mkoa wa Kinondoni kwenye
fainali za Taifa upande wa wanaume na nafasi ya pili ilichukuliwa na
Mohamed Idd ambaye alizawadiwa Shilingi 250,000/=
Mchezaji mmoja mmoja Wanawake, Grace Thomas alifanikiwa
kutwaa ubingwa huo na kuzawadiwa fedha taslimu Shilingi 300,000/
= pamoja na kuwakilisha mkoa katika fainali za kitaifa upande
wa wanawake.Nafasi ya pili ilichukuliwa naCecilia Kileo ambaye
alizawadiwa fedha taslimu Shilingi 200,000/=.
Fainali za kitaifa za 2014 za “Safari National Pool Competion”
zinatarajiwa kufanyika Moshi Mkoani Kilimanjaro kwa
kushilikisha Mikoa 17 ambayo ni Tabora,Shinyanga,Dodoma
Mbeya,Iringa,Morogoro,Mwanza,Kagera,Manyara,Arusha,Tanga,Pwan
i,Ilala,Lindi,Temeke,Kinondoni na wenyeji wa mashindano kwa mwaka
huu mkoa wa Kilimanjaro.
Wachezaji wa timu ya Top Land wakishangilia kwa kucheza na kitita cha Shilingi 800,000/= mara baada ya kuibuka mabingwa wa mashindano ya Safari Pool 2014 kwa Mkoa wa kimichezo wa Kinondoni jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Katibu Mkuu wa Chama cha Pool Taifa, Amos Kafwinga akimkabidhi Nahodha wa timu ya Top Land kitita cha fedha taslimu Shilingi 800,000/ = mara baada ya kuibuka mabingwa wa mashindano ya Safari Pool 2014 kwa Mkoa wa kimichezo wa Kinondoni jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...