Na Asteria Muhozya, Mbinga
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi amewataka
watanzania kuondoa dhana kuwa madini yanayochimbwa katika migodi
mbalimbali nchini yanaibwa na wawekezaji wakubwa na kusisitiza kuwa,
Wizara kupitia Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA), wapo
katika migodi yote nchini kuhakikisha kwamba madini hayo hayatoroshwi .
Maswi ameyasema hayo alipotembelea Mgodi wa kuchimba Makaa
ya Mawe wa kampuni ya Tancoal eneo la Ngaka wilayani Mbinga
inayomilikiwa kwa ubia kati ya Kampuni ya Australia na Shirika la
Maendeleo ya Taifa (NDC) na kuongeza kuwa, TMAA wapo katika kila
mgodi kujua kiasi cha madini kinachochimbwa, kinachouzwa na kwa ajili
ya kuhakiki vyeti vya mauzo ya madini hayo kuhakikisha kuwa vinakwenda
sambamba na kiasi cha mrahaba kinachotolewa na wawekezaji.
Kwa upande wake Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Paul Masanja
alisisitiza hoja ya Katibu Mkuu Maswi na kuongeza kuwa, Wizara kupitia
maafisa wa TMAA wamekuwa wakifanya ukaguzi kuhakikisha kwamba
serikali inapata mrahaba stahili kupitia madini yanayouzwa na kutoa mfano
kwa madini ya Makaa ya Mawe ya Ngaka kwamba serikali inapata asilimia
100 ya mrahaba.
“Nawapongeza sana TanCoal ni wasikivu, maafisa wa TMAA huwa
wanafanya ukaguzi kila baada ya miezi mitatu kujua kiasi kinachozalishwa
na kinachouzwa hivyo, tunakwenda nao vizuri,” alisisitiza Masanja.
Naye Mkurugenzi wa Tancoal Tan Brereton ameeleza kuwa, mgodi wa
wa Ngaka ni mradi mkubwa kwa Tanzania na kuongeza kuwa, uwepo
wa mgodi wa makaa ya mawe wa Tancoal ni mafanikio na maendeleo
makubwa kwa Tanzania kutokana na kuwezesha ajira kwa wataalamu
mbalimbali nchini ikiwemo serikali kupata kodi na mirahaba kupitia mgodi
huo jambo ambalo litawezesha kuboresha huduma za kijamii.
Aidha, amezitaja faida za nyingine za mgodi huo kuwa, uwepo wa Mgodi
huo utawezesha Tanzania kuzalisha kiasi kikubwa cha nishati ya umeme
kutokana na uwepo wa kiasi kikubwa cha makaa hayo katika mgodi wa
Ngaka na kueleza kuwa, makaa ya mawe kutoka katika mgodi huo yana
ubora wa kiwango cha juu tofauti na madini yanayochimbwa nchini Afrika
Kusini.
“Makaa ya Ngaka yana ubora wa hali ya juu sana tofauti na makaa ya
nayochimbwa Afrika Kusini kwasasabu madini haya hayahitaji kusafishwa
kabla ya matumizi tofauti na mengine ambayo husafishwa kabla ya
kutumiwa ,alisisitiza Tan.
Aidha ameongeza kuwa, kampuni hiyo ina uwezo wa kuzalisha kiasi cha
tani 480,000 za makaa ya mawe kwa mwaka na kuongeza kuwa, tayari
kampuni hiyo imesaidia huduma mbalimbali za kijamii katika maeneo ya
afya,shule ,maji na kuwaendeleza vijana na kutumia zaidi ya shilingi milioni
mia sita na kuongeza kuwa, kampuni hiyo imekwisha toa kiasi za bilioni 2
kama kodi na mrahaba kwa serikali.
Kwa mujibu wa Tan, ameeleza kuwa, makaa yanayozalishwa na kampuni
hiyo yanatumika katika viwanda vya saruji vya Mbeya Tanga Lake,
kampuni ya METL na viwanda vya karatasi viwanda vya nguo.
Mashine ya kusaga makaa yam awe katika viwango mbalimbali kulingana na mahitaji ya wateja ikiendelea na kazi ya kusaga mawe katika Mgodi wa Mkaa ya Mawe wa Ngaka unaomilikiwa kwa ubia na Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) na kampuni ya Australia.
Gari la kubeba makaa ya Mawe katika mgodi wa Ngaka likimwaga makaa sehemu maalum kutoka mgodini kabla ya kusagwa katika viwango mbalimbali kulingana na mahitaji y wateja.
Meneja wa Kampuni ya TANCOAL (wanne kulia) Tan Brereton na Mkuu wa Masoko wa kampuni hiyo Emmanuel Constantinides (wa tatu kulia) wakimwonesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi na ujumbe wake namna shughuli za himbaji Makaa ya Mawe zinavyofanyika.
Gari la kubeba kupakia Makaa ya Mawe likiendelea na kazi hiyo katika Mgodi wa Ngaka unaomilikiwa na kampuni TANCOAL.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...