Askofu
wa kanisa la Evanglist Assembels of God Tanzania (E.A.G.T) Singida
mjini, John Mafwimbo akizungumza kwenye mkutano wa Injili uliofanyika
kwenye viwanja vya shule ya msingi Ukombozi mjini Singida.Pamoja na
mambo mengi, askofu Mafwimbo amewasihi wajumbe wa Bunge Maalum la
Katiba, kufanya mambo waliyotumwa na Watanzania na si vinginevyo.
Na Nathaniel Limu, Singida
Makanisa
ya Kipentekoste mkoani Singida, yameungana na Watanzania wengine
kuwaomba wajumbe wa Bunge Maalum la kuandaa Katiba mpya,kujiepusha na
mambo/vitendo ambavyo hawakutumwa na wananchi na badala yake washikamane
na wavumiliane ili waweze kufanikisha kupatikana kwa katiba
itakayoendeleza amani na utulivu uliopo nchini.
Makanisa
hayo ambayo ni pamoja na Free Pentekoste Tanzania na Evangelist
Assembles of God Tanzania (E.A.G.T.),yamedai kwamba matusi, dharau,
ugomvi na kejeli za aina mbalimbali hazitachangia kupatikana kwa Katiba
inayotarajiwa na Watanzania.
Wamedai
vitendo hivyo, vitachangia pamoja na mambo mengine kubomoa umoja na
undugu uliojengeka kwa miongo mingi na vitakaribisha vitendo viouvu kama
vinavyofanywa na vikundi vya Boko haramu na Alshabab.
Akizungumza
kwenye mkutano mkubwa wa injili uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya
msingi Ukombozi mjini Singida, Askofu wa E.A.G.T, John Mafwimbo alisema
ni wakati sasa kwa waumini wa madhehebu mbalimbali ya dini kufunga kwa
ajili ya kufanya maombi kuliombea Bunge Maalum la Katiba,liweze
kutekeleza yale yote waliyotumwa na Watanzania.

Mchungaji
wa kanisa la Free Pentekoste Tanzania Singida mjini, Boniface Ntandu,
akiwahubiria waumini wa madhehebu ya dini mbalimbali waliohudhuria
mkutano wa injili uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi
Ukombozi.
"Tuwaombee
bila kuchoka wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba,waweze
kututengenezea/kutuboreshea vizuri Katiba na wala wasituchanganye,ili
sisi huku waumini wa madhehebu ya dini na Watanzania wengine wasiokuwa
na dini tuje tufanye uamuzi sahihi wakati wa kuipigia kura Katiba
hiyo",alifafanua.
Akifafanua
zaidi, Mafwimbo, alisema kazi ya wajumbe nikuwajengea Watanzania
mazingira mazuri ili waje kupigia kura Katiba itakayokidhi mahitaji yao
ya zaidi ya miaka 50 ijayo.
Kwa
hali hiyo, Askofu Mafwimbo amewashawishi wajumbe hao kuimarisha
utamaduni wa kuvumiliana, kupendana na kumaliza tofauti zao wao kwa wao.
"Niwakumbushe
tu wajumbe wetu, kwamba Watanzania ni waumini wazuri wa amani na
utulivu. Kitendo hicho kimeendelea kuchangia nchi yetu kupaa kimaendeleo
na wakati huo huo, sisi waumini tunaendelea kuabudu kwa uhuru mpana
bila usumbufu wa aina yo yote",alisema na kuongeza kwa kusema; "Endapo
hatutapata katiba stahiki,tutakuwa tunakaribisha vurugu kama zile
zinazofanywa na makundi ya boko haramu".

Moja
ya kwaya zilizokuwa zikihubiri kwa njia ya nyimbo kwenye mkutano wa
injili ulioandaliwa na mwimbaji wa nyimbi za injili mkoa wa Singida,
Elineema Babu.

Baadhi
ya waumini wa madhehebu mbalimbali ya dini,waliohudhuria mkutano wa
injili unaoendelea kwenye viwanja vya shule ya msingi Ukombozi mjini
Singida.(Picha zote na Nathaniel Limu).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...