Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda (katikati) katika picha ya pamoja na Rais wa
Samoa, Bw. Tui Atua Tupua Tamasese (kulia) na mkewe Bibi Filifilia Tamasese (Agosti 12, 2014). Wa pili kushoto ni Katibu
Mkuu wa Universal Peace Federation (UPF), Bw. Tageldin Hamad ambao wameandaa mkutano huo.
Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda (katikati) katika picha ya pamoja na Katibu
Mkuu wa Universal Peace Federation (UPF), Bw. Tageldin Hamad (kushoto) ambao wameandaa mkutano huo. Kulia ni Dk. Amalberga Kasangala
kutoka Tanzania ambaye pia anashiriki mkutano huo
Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda akiwa na Rais wa Universal Peace Federation (UPF), Dk. Thomas Walsh (kushoto) na wajumbe
wengine wanaoshiriki Mkutano wa Dunia kuhusu Amani na Usalama unaoendelea
jijini Seoul, Korea Kusini.
Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda akiwa na wajumbe wengine kutoka Afrika Kusini,
Japan na Marekani ambao wanashiriki Mkutano wa Dunia kuhusu Amani na Usalama unaoendelea
jijini Seoul, Korea Kusini. (PICHA NA
IRENE BWIRE WA OWM).
Baadhi ya wajumbe kutoka Kenya, Tanzania
na Lesotho ambao wanashiriki Mkutano wa Dunia kuhusu Amani na Usalama unaoendelea
jijini Seoul, Korea Kusini. (PICHA NA
IRENE BWIRE WA OWM).
Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda akifuatilia
matukio kwenye ukumbi wa Mkutano wa Dunia kuhusu Amani na Usalama unaoendelea
jijini Seoul, Korea Kusini. Wa pili
kulia ni Rais mstaafu wa Mali, Prof. Dioncounda Traore. Wa kwanza kushoto ni
Rais wa Samoa, Bw. Tui Atua Tupua Tamasese na mkewe Bibi Filifilia Tamasese.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...