Wizara ya Nishati na Madini kupitia Kitengo cha Uthamini wa Madini ya Almasi na Vito
(TANSORT) inatarajia kufanya semina ya siku mbili ambayo itahusisha Makamishna
Wasaidizi wa Madini wa Kanda na Afisa Madini Wakazi yenye lengo la kujadili
utendaji kazi, mafanikio pamoja na maboresho ya tasnia ya vito na almasi nchini.
Semina hiyo itakayofunguliwa na Katibu Mkuu wa Wizara Bw. Eliakim Maswi,
inatarajiwa kuanza Agosti 14, 2014 na kumalizika Agosti 15, 2014.
TANSORT itaendesha semina hiyo ili kuboresha shughuli za uthamini wa almasi na
madini ya vito kwa lengo la kukokotoa mrabaha, kutayarisha miongozo ya bei za
madini zinazotumika kukokotoa mrabaha, kutoa huduma za kijemolojia ( Gemological
Services) kwa wachimbaji wadogo na wa kati, kusimamia mauzo ya almasi na madini
ya vito ndani na nje ya nchi.
Semina hiyo itawawezesha washiriki kutoa maoni yatakayowezesha Kitengo hicho
kuboresha huduma za kutoa ushauri wa masoko, ukataji na ukadiriaji thamani kwa
wachimbaji wadogo na wa kati, kufanya utafiti wa masoko na bei za almasi na madini
ya vito, kutunza takwimu za uzalishaji na mauzo ya almasi na madini ya vito na
kusimamia tasnia ya almasi na madini ya vito nchini.
Kitengo cha TANSORT kilianzishwa mwaka 1966 malengo yake yakiwa ni pamoja na
kusimamia mrabaha stahiki unaokusanywa na kulipwa serikalini na kuhakikisha madini
ya almasi na vito yanayozalishwa nchini yanapata bei bora.
Imetolewa na:
WIZARA YA NISHATI NA MADINI
12 Agosti, 2014
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...