Maofisa wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) wanawasili nchini kesho (Agosti 10 mwaka huu) kuangalia jinsi mchezo huo unavyoondeshwa nchini.
Ujumbe huo wa FIFA utakaokuwa na maofisa sita, baada ya ziara yake utashauri jinsi ya kuboresha uendeshaji huo katika kikao cha pamoja kati yake na Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kitakachofanyika mwishoni mwa wiki ijayo.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...