Mkulima (wa pili kulia) wa Shayiri katika mashamba ya Monduli Juu, wilayani Monduli mkoani Arusha akiendelea na uvunaji wa Shayiri kwa kutumia mashine ya kisasa ambapo wameweza kuvuna hadi gunia 1o kwa hekari moja. Wakulima wa Monduli Juu wameanza kuvuna mazao yao, baada ya kuwezeshwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) iliyowapatia mafunzo, mikopo ya mbolea na dawa. Pia shayiri hiyo hununuliwa na TBL kwa ajili ya kutengenezea kimea katika kiwanda kilichopo Moshi, mkoani Kilimanjaro.
 Afisa Ugani wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Monduli Juu na West Kilimanjaro, Editha Temu akipima kuangalia ubora wa Shayiri iliyoanza kuvunwa katika mashamba ya Monduli Juu. Kushoto ni  ni Mwenyekiti wa wakulima wa Shayiri Monduli Juu Bariki Kivuyo.


 Mkulima wa Shayiri Goigoi Kivuyo akionyesha sehemu ya shamba linalotarajiwa kuvunwa Shayiri eneo la Monduli Juu, wilayani Monduli mkoani Arusha, baada ya kulima kwa kufuata maelekezo na mkopo  wa mbegu na dawa kutoka Kampuni ya TBL
: Mkulima wa mfano Mepoloo Lolosi aliyelima hekari 180 za Shayiri katika eneo la Monduli Juu wilayani Monduli, mkulima huyo alikuwa akionyesha baadhi ya zana za kilimo ambazo aliwezeshwa kuzipata kwa njia ya mkopo ili kufikia malengo yake ya kulima kisasa.  Tayari amekwisha kumaliza kuzilipia zana hizo pamoja na nyingine.
Meneja wa Barley kutoka  Kiwanda cha Bia nchini (TBL) Dk. Bennie Basson akiwaonyesha waandishi wa habari hawao pichani namna Kampuni hiyo inavyowawezesha wakulima wa Shayiri katika kulima kilimo bora chenye tija.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Barley kutengeneza ulevi...tulewe..wapate faida wawekezaji eti wanatozwa kodi...kodi gani; uduchu!

    Afadhali wanelima ngano!

    ReplyDelete
  2. Mfano mzuri wa kufanikisha KILIMO kwanza kuanzia mbegu, ukulima wa kisasa, pembejeo na soko la uhakika.

    Serikali kuu, wizara ya kilimo, serikali za mitaa na wadau mbalimbali wanaweza kujifunza mengi toka ushirikiano wa mafanikio wa TBL na wakulima wa shairi na kufanya mapinduzi ktk kilimo cha chakula na matunda.

    Hapa hakuna haja ya kwenda nje ya nchi kujifunza bali waende Monduli kuangalia wakulima na TBL wamefanikiwa vipi ktk KILIMO KWANZA kwa vitendo viletavyo manufaa kwa wadau wote.

    Mdau
    Christos Papachristou
    Diaspora.

    ReplyDelete
  3. Safi sana TBL hivi ndivyo tunavyoweza saidia jamii kupambana na umaskini kwa kuwawezesha kulima mazao ya biashara lakini wakiwa na uhakika wa masoko
    Hongera Afisa Ugani kwenye hiyo picha Bi Editha Temu....tunahitaji wataalamu wazalendo kama wewe mnaopambana hapo mlipo na mkiwa tayari kusaidia jamii

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...