Baada ya kuona kuwa kuna maeneo mbalimbali ya vivutio vya kitalii muhimu na ambavyo vimesahaulika kwa njia moja au nyengine na pengine hakuna pa kuvitangaza ili watanzania na Dunia kwa ujumla wapate kuvifahamu kwa ukaribu , Tone Multimedia Group kupitia mtandao wake wa Mbeya yetu Blog wameamua kuanza rasmi kuvitembelea na kutangaza kwa Jamii kwa ujumla wapate kuvifahamu ili nao waje kuvitembelea.
Safari hiyo ambayo moja kwa moja ilianzia Mkoa wa Mbeya Wilaya ya Rungwe-Tukuyu kwenda kujionea vivutio hivyo mbalimbali kikiwepo cha kwanza kabisa ambacho ni Kijungu eneo ambalo ni la kipekee na lenye historia ya aina yake.
Hivi ndivyo safari ilivyokuwa Fuatilia hapa kwa makini.
Kwanza kabisa tulifika katika kibao hiki ambacho kimetoa maelezo ya awali ikiwa ni pamoja na Bei ambazo mtu anatakiwa kutozwa wakati anapotaka kuingia katika eneo hilo, Bei hizo zimewekwa na uongozi wa Serikali ya Kijiji ambapo fedha hizo zinasaidia katika mambo mbalimbali za kuendeleza kijiji hicho ingawa hata hivyo kuna changamoto kadha wa kadha ambazo zinawakabili ikiwa ni pamoja ni Gharama kubwa za kuingia katika eneo hilo kwa wazawa ambapo haichagui kwamba umetoka nje ya nchi au ndani Jambo ambalo Serikali inapaswa kutazama kwa sababu ni zaidi hata ya kuingia katika Hifadhi za Taifa.
Picha hii ilipigwa kwa juu kabisa kuonesha Jinsi eneo la Kijungu linavyo onekana
Hapa ni eneo ambalo Maji ya mto huo yanatokea katika eneo linaitwa Namba One eneo la ukanda wa juu kabisa wa eneo hilo, Majihayo pamoja na mengine mengi hata wakati wa mvua kubwa ni lazima yazunguke yanapo kwenda lakini mwisho wa siku ni lazima yaishie hapa, Pia hapa ndipo maji haya yanapoanza kutililikia moja kwa moja katika kijungu.
Well done. But I think Elimu inanze na alieyeandika hili Bango.
ReplyDelete