Na Magreth Kinabo, MAELEZO Dodoma 
 Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Mhe Said Arfi (pichani) ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA)amezitaja sababu za kurejea katika bunge hilo, kuwa ni hofu ya Mwenyezi Mungu. 
 Aidha Mhe Arfi ameitaja sababu nyingine ni kwamba amerudi katikaBunge hilo, ili kuhakikisha kwamba anaisadia nchi kupita katika mchakato wa Katiba mpya kwa amani na utulivu kwa kutumia kipaji chake na kuwatumikia Watanzania. 
 Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na mjumbe huyo, wakati akihojiwa na kipindi cha Jambo Tanzania kinachorushwa na Shirika la Utangazaji la Tanzania(TBC). 
Akizungumza katika kipindi hicho, huku akinukuu kitabu cha Nabii Musa, Arfi alisema Mwenyezi Mungu hawapendezwi na mtu mwenye jeuri na anayejivuna. “Nimejitathimini na kuona mimi mwenyewe ni nina nafasi gani… maaskofu, mapadre, wachungaji na masheikh. Viongozi wetu wametusihi turudi turudi napata kiburi wapi cha kutokurudi,” alihoji Mhe Arfi. 
 Akirejea katika kitabu cha Qruan anasema Mwenyezi Mungu hapendezwi na mtu mwenye kiburi na anayejivuna. 
 Aliongeza kuwa viongozi hao “ wana nafasi kubwa pia wanaheshima ndio maana nimeweza kurudi,"”alisema. Mjumbe huyo alisema sasa ni wakati wa kila mtu kueleza ukweli, kwani amerejea katika Bunge hilo, amepata bahati ya kuchangia katika sura ya nne katika kifungu cha 43na 44 kinachohusu haki za msingi.
 “Nimepata fursa ya kutoa mapendekezo ya haki za wazee nisingewezakuwasilisha kama ningekuwa nje. Pia haki za wafanyakazi,” alisema. 
 Akizungumzia kuhusu wajumbe wenzake waliosusia Bunge hilo, aliwataka kutanguliza maslahi ya taifa.Huku akisisitiza kwamba atajitahidi kuwashawishi wajumbe walioko nje ya Bunge hilo ili waweze kurejea. Arfi aliwahakikishia wananchi kuwa wanawatengenezea Katiba itakayowasaidia kubadilisha ya watu wote.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. The mdudu,amakweli njaa mbaya sn yaani maneno anavyoyapangilia utasema hachukui hiyo posho ya LAKI 3 kwasiku yaani amewazunguuka wenzake kwa laki tatu kisha anamshilikisha mungu na kitabu chake takatifu,hawa ndio mamluki wenyewe tuwe makini na watu kama hawa.

    ReplyDelete
  2. Siasa ni kusema uongo tu

    ReplyDelete
  3. Perfect sense. Siasa sio nguvu ni mbinu. Mwamuzi Wa mwisho ni mwananchi...

    ReplyDelete
  4. Hata mie sikufurahia na nukuu zake........ngoja tuone mwisho .....nadhani kuna watakao ficha sura zao kwa aibu...ndivyo ilivyo ktk njia yenye makorongo na shida nyingi lazima kuna wenza utawaacha tu njiani.....

    ReplyDelete
  5. Mchangiaji hapo juu-Anonymous 08.11.14 unapaswa kufahamu kuwa kila mtu anahaki wa kuchambua,na kutoa maamuzi yake kadri anvyoona hali halisi. Kutokuwepo kwa Ukawa ndani ya bunge la katiba kunatija gani kwa wananchi.Je,Ukawa wameshindwa kurejea kwa masharti? na vile x2 kutokuwepo katika bunge hili ni sawa na kuwapa CCM a greelight kupitisha kila watakaloliona linafaa.Je, Ukawa hawaoni kuwa wanapoteza haki zao na za Watanzania kwa ujumla kwa kushindwa kuwakilisha mawazo yetu?
    Binafsi sioni kama ni busara kwa Ukawa kuendelea kugoma.

    ReplyDelete
  6. Karibu bungeni mh Arfi, huo ndio uungwana tunataka viongozi wetu mupangilie mambo ya maana kuhusu maisha yetu. Hapana mtu kuongelea mambo ya serikali ngapi kutuongezea mzigo usio bebeka kwa sababu kuna watu wanataka madaraka

    ReplyDelete
  7. Mimi nafikiri ametambua kosa lake na zaidi hofu ya Mungu ndo iliyomsukuma. Kila mtu atahukumiwa yeye peke yake hii ya kufuata sijui fulani kasema tusifanye hivi or vile itawapeleka pabaya. Kukaa nje kwa wawakilishi wa chadema hakutafanya suluhisho la katiba bali malumbano na fitina zaidi. Ni heri kumuogopa Mungu kuliko kushupaa na dhamila yako. Mimi nampongeza kwa maamuzi yake.

    ReplyDelete
  8. astaghafiru llah, unatisha voo babu kujifanya huijuwi Latina yetu, hio ni kudanganya watu, cna umerudi kufuata Hiyoo posho huna kengine.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...