Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote(EOTF), Mama Anna Mkapa akitoa neno la shukrani kwa wahisani wakati wa hafla ya kukabidhi vitabu kwa ajili ya kusaidia shule 45 na vyuo 3 vilivyotolewa na Books for Africa kutoka nchini Marekani leo jijini Dar es Salaam,kushoto ni Mwakilishi kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Bibi.Paulina Mkonongo na katika ni mwakilishi wa Balozi wa Nigeria nchini Bibi. Abiola Delupe.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote(EOTF), Emmanuel Matee akielezea historia ya mfuko huo kwa wadau mbalimbali wa elimu katika hafla ya kupokea vitabu kwa ajili ya shule za Msingi, Sekondari na Elimu ya Juu vilivyotolewa na Books for Africa kutoka Marekani leo jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF), Mama Anna Mkapa akimkabidhi kitabu mwakilishi wa Shule ya Sekondari Overland, iliyopo Kisarawe ndg. Allison Sila wakati wa hafla ya kukabidhi vitabu kwa ajili ya kusaidia shule 45 na Vyuo 3 vya Elimu ya Juu vilivyotolewa na Books for Africa kutoka nchini Marekani na kusafirishwa kwa hisani ya Mfuko wa Sir. Emeka Offod wa nchini Nigeria leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF), Mama Anna Mkapa akiwa katika picha ya pamoja na wadau pamoja na wahisani wa Elimu wakati wa hafla ya kukabidhi vitabu kwa ajili ya kusaidia shule 45 na Vyuo 3 vya Elimu ya Juu vilivyotolewa na Books for Africa kutoka nchini Marekani na kusafirishwa kwa hisani ya Mfuko wa Sir. Emeka Offod wa nchini Nigeria leo jijini Dar es Salaam. Picha na MAELEZO
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...